Baada ya kukwaruziwa au kuharibiwa gari yako ulichukua uamuzi gani kwa mhusika?

G Tank

JF-Expert Member
Joined
Feb 9, 2023
Posts
2,297
Reaction score
8,760
Nakumbuka hapo cha miaka ya 2013 niliwahi kuwa kwenye foleni ya barabara ndogo tunasubiri kuingia barabara kuu , Ghafla nikahisi kishindo kizito kwenye buti, kuagalia nyuma ni gari aina ya mark 2 Grande imeparamia.

Sikupoteza muda nilishuka na sura ya kazi nikaifuata gari iliyoparamia, Kulikuwa na kijana age kama 25 kwa mbali niliona kama ana hofi lakini alikuwa mstaarabu alikiri kosa hivyo nikamwambia twende eneo la karibu la wazi tukayakenge.

Mara ya kwanza alisema tukairekebishe gari kwa fundi wake lakini nilikataa kwasababu nina mafundi wangu walio karibu na eneo la tukio, nashukuru tena kijana alikuwa mstaarabu hivyo tuliongozana hadi garage, fundi akapiga hesabu ni elf 80.

Kijana akaniambia anaenda kuitoa mpesa niliiacha gari yangu garage tukapanda yake, kufika kwa wakala tukamalizana nikarudi garage na kumaliza shughuli.
 
Jumamosi ya tarehe 30 mwezi wa tisa mapema tu niliibamiza crown athlete ya watu nikiwa na canter maeneo ya posta sikufanya hiyana nikaenda ilala nikanunua taa mpya ya nyuma nikamuekea maisha yanasonga na yule muhindi jambo la kushukuru ingawa imenitoka laki mbili lakn nimetengeneza urafiki na muhindi na baadhi ya michongo ya mizigo napata.
 
Niligongwa kwa nyuma mitaa ya Kigogo na kijana akiwa kwenye gari na mpenzi wake na gari lenyewe kaazima kwenda shopping ya Christmas 2022, nilishuka nikamwambia tuelewane atengeneze, akawa hana fedha, akamuomba mpenzi wake akapewa Tshs 7000 (Elfu 7), akapiga simu kwa jamaa zake hakupata kitu, akampigia mwenye gari, naye hakumsaidia zaidi ya kumlaumu kwa uzembe, nikabadilika usoni macho yakawa mekundu ghafla nikamwambia shika chini akalala haraka kwa hofu, nikachukua kiboko nikantandika fimbo 3 mbele ya mpenzi wake na kumwambia awe makini barabarani, nikaondoka zangu
 
Nakumbuka hapo cha miaka ya 2013 niliwahi kuwa kwenye foleni ya barabara ndogo tunasubiri kuingia barabara kuu , Ghafla nikahisi kishindo kizito kwenye buti, kuagalia nyuma ni gari aina ya mark 2 Grande imeparamia.

Sikupoteza muda nilishuka na sura ya kazi nikaifuata gari iliyoparamia, Kulikuwa na kijana age kama 25 kwa mbali niliona kama ana hofi lakini alikuwa mstaarabu alikiri kosa hivyo nikamwambia twende eneo la karibu la wazi tukayakenge.

Mara ya kwanza alisema tukairekebishe gari kwa fundi wake lakini nilikataa kwasababu nina mafundi wangu walio karibu na eneo la tukio, nashukuru tena kijana alikuwa mstaarabu hivyo tuliongozana hadi garage, fundi akapiga hesabu ni elf 80.

Kijana akaniambia anaenda kuitoa mpesa niliiacha gari yangu garage tukapanda yake, kufika kwa wakala tukamalizana nikarudi garage na kumaliza shughuli.
Nilimpa hela ya usumbufu wa kukwaruza gari lake na langu
 
Mimi nilikuwa sayansi jioni, nyuma kuna gari nadhani ilikuwa spacio old model. mara ikatoka huko gari speed ikamgonga wa nyuma yangu naye akanigonga mimi. Kushuka anashuka jamaa zip imefunguliwa amelewa na jimama sijui lilikuwa linamnyonya mkuyenge.
Basi yule jimama ndio akaanza kuongea, trafiki alikuwa karibu akawa amefika. maza akataka tumalizane na trafiki akasema kama tunamalizana tumalizane lakini yule binti wa spacio akataka pesa ndefu sijui milioni, maana alimpgia mzee wake mwanajeshi mstaafu ana mikwara balaa. Basi yule jimama akasema halipi sote twende huko huko polisi tufuate utaratibu wa kawaida maana hawezi nilipa mimi halafu bado huyu mmoja amkomalie.
Sasa mimi sikuwa na leseni, ikabidi nisepe zangu tu na kuiepeleka mwenyewe garage nikainyoosha na kurudisha rangi kwa lak mbili hivi. Na gari ilikuwa ina siku kama 5 toka nimenunua nilihisi roho inataka kunichomoka.
 
Niligongwa kwa nyuma mitaa ya Kigogo na kijana akiwa kwenye gari na mpenzi wake na gari lenyewe kaazima kwenda shopping ya Christmas 2022, nilishuka nikamwambia tuelewane atengeneze, akawa hana fedha, akamuomba mpenzi wake akapewa Tshs 7000 (Elfu 7), akapiga simu kwa jamaa zake hakupata kitu, akampigia mwenye gari, naye hakumsaidia zaidi ya kumlaumu kwa uzembe, nikabadilika usoni macho yakawa mekundu ghafla nikamwambia shika chini akalala haraka kwa hofu, nikachukua kiboko nikantandika fimbo 3 mbele ya mpenzi wake na kumwambia awe makini barabarani, nikaondoka zangu
Haha yani kabisa umtandike fimbo? Huyo alikuwa mtoto mdogo labda
 
Miezi kama mitatu imepita, Fuso moja la abiria(zile injini nyuma ) lilipitia sight mirror huko mbagala kwenye zile double road..

Cha ajabu jamaa wa Fuso akaanza kunikejeli wakati yeye ndiyo mwenye makosa. Aisee nilimletea kizaa zaa yule bwana hawezi sahau.

Baada tu yakumalizana nae, wakati naingia tu barabarani nikajipata nimeigonga Forester xt ya mama mmoja hivi..

Nashukuru yule mama alinisamehe akanisihi nipunguze hasira maana yanaweza kunikuta makubwa zaidi!!!
 
Mimi nilikuwa sayansi jioni, nyuma kuna gari nadhani ilikuwa spacio old model. mara ikatoka huko gari speed ikamgonga wa nyuma yangu naye akanigonga mimi. Kushuka anashuka jamaa zip imefunguliwa amelewa na jimama sijui lilikuwa linamnyonya mkuyenge.
Basi yule jimama ndio akaanza kuongea, trafiki alikuwa karibu akawa amefika. maza akataka tumalizane na trafiki akasema kama tunamalizana tumalizane lakini yule binti wa spacio akataka pesa ndefu sijui milioni, maana alimpgia mzee wake mwanajeshi mstaafu ana mikwara balaa. Basi yule jimama akasema halipi sote twende huko huko polisi tufuate utaratibu wa kawaida maana hawezi nilipa mimi halafu bado huyu mmoja amkomalie.
Sasa mimi sikuwa na leseni, ikabidi nisepe zangu tu na kuiepeleka mwenyewe garage nikainyoosha na kurudisha rangi kwa lak mbili hivi. Na gari ilikuwa ina siku kama 5 toka nimenunua nilihisi roho inataka kunichomoka.
Watu mna hatari yan unamiliki gari mamilion na hauna leseni bhs hata ya kununua tu hii ni maajabu
 
Dah haya mambi basi tu omba yasikukute kuwa umemparamia aidha mtu ambaye ndio amemiliki gari kwa mara ya kwanza au mtu alieazima gari utaona dunia chungu.
Kwa maa ya kwanza nilimkwaruza jamaa kidg ila nlikuwa namfaham yeye hanifaham hakunimaind ila alisimama akanambia niwe makin kwa kuwa nisingweza gharam ya rangi.
Mara ya pili nilipasua taa ya mshkaji moja hiv kumbe gari ni ya jimama lake mamamaaaaaa sitosahau
 
Hata zile lesen za karatasi za miezi 3 hukupatiwa kipind unasubiria lesen mkuu!?
Mkuu ilikuwa unalipa unasubiri lesen sikuwa nmekwenda driving. Ukilipa unaenda chukua lesen nadhan baada ya siku 5 kama sijasahau
 
Nilikwaruzaga k passo cha mtu kwenye pantoni nikataka nimpe 30k akakomaa anataka 70k. Tukafikishana police kigamboni.. Nilimuuliza trafik kama Road Traffic Act, 1978 Ina apply mpaka majini. Alikaa kimya pamoja na mgongwaji. Nikawasha Gari nilaenda zangu sun set kunywa beer za mchana.
 
Back
Top Bottom