NetMaster
JF-Expert Member
- Sep 12, 2022
- 1,454
- 4,925
Muda hausimami, muda ukifika wa ku hit the road inakubidi uondoke nyumbani kwenu nawe uanze kujitafutia.
Wapo wanaohama wakiwa na mishe ila wapo pia ambao ni kuhama na kuyajua mbele kwa mbele
Binafsi nakumbuka nilipomaliza form 4, nilikaa kitaa nikiwa nasubiri matokeo bila shughuli yoyote zaidi ya kushinda vijiweni, kufukuzia videm, kucheki muvi, kuzurura mitaani, n.k.
Matokeo yalipotoka hayakuwa mazuri,
Nilibaki home, Mzee aliniambia kama sina cha kufanya nijandae mwakani niende kijijini kumsaidia mjomba kulima, Aweeee!! nikaona huko ndio mwanzo wa kuwa mwanakijiji hadi uzeeni, kijijini huko hata umeme tu ilikuwa ni ishu.
Ilibidi nizuge zuge pale home, huku nyuma ya pazia nikaanza kujifunza useremala, hakuna cha nauli ni mwendo wa kukanyaga tu, huko ofisini wazoefu nao wapo wasio na utu yani ukosee kidogo tu ma uombe kufundishwa mara mbili ni matusi ama kukutania mpaka basi.
Ndani ya mwaka hivi miezi 8 hivi nikaanza kukabidhiwa vikazi vidogo vidogo ila hela ndogo sana, baada ya mwaka ndio walau nikaanza kupata vidili si haba,, muda huo mzee kaanza kunikumbusha kabisa nijiandae kwenda kijijini.
Ilibidi nihame tu hapo home, kuanzia muda huo ndio zikawa shughuli zangu hizo hizo mpaka leo hii.