Baada ya kupima UKIMWI leo

Baada ya kupima UKIMWI leo

Rk10

JF-Expert Member
Joined
Apr 6, 2015
Posts
1,216
Reaction score
1,372
Wanajamii habari za Leo.
Leo juma tatu tareh 19/03/2018 nimeenda na Mke wangu kupima ukimwi baada ya kuwa na mimba ya miezi sita. Kiukweli hili jambo la kupima ugonjwa huu siyo rahisi kabisa na linaitaji ujasili Wa hali ya juu sana.
Nikiwa mapokezi nimeona watu wakitoka kwa uzuni mkubwa sana na wengine wakibubujikwa na machozi.

Nikiwa pale kwenye foleni mapokezi nimewakumbuka wanawake wote niliozini nao tena kwa mtiririko mzuri kabisa kuanzia Wa kwanza hadi Wa mwisho.

Wanawake hao nimewaweka kwenye makundi mawili niliotumia kinga na ambao sikutumia kinga kabisa. Kwa ambao sikutumia kina nimeanza kuchambua mmoja mmoja na hapa ndo nilitamani kukimbia majibu kwa sababu wengine nilikuwa siwaamini kabisa.

Muda uliwadia Wa Mimi na wife kuingia, tulifanya vipimo na baadae tukaambiwa tusubili hapa ndo kuna kazi sasa maana nililowa jasho mwili mzima huku akili yangu ikiniambia nitoke nduki wife atakuja na majibu home, lakini moyo ukasema vumilia liwalo na liwe.

Baada ya dakika chache tukaitwa na wala hatujapewa ushauli na saha, tulivyofika pale wakati natetemeka tukapewa majibu na tukaambiwa tuko salama na tukapewa majibu yetu pale tukawa na bashsha pale. Kiukweli nimefurahi sana baada ya kupata majibu.

Hii itanisaidia kuishi kwa taadhari sana katika maisha yangu ili niweze kuilea na kuishi na familia yangu vizuri.

Ushauri
Kupima ukimwi kunaogopesha sana lakini kunafaida nyingi sana za kupima nimeziona.
1. Kutambua afya yako.
2. Kuna watu wanaishi maisha ya kukata tamaa wakidhani wamesha athirika kumbe wapi.
3. Hata ukikuta umeathirika utajua ufanye nini ili uishi muda mrefu zaidi.

TWENDE TUKAPIME TUZIJUE AFYA ZETU HATA KAMA JAMBO HILI LINAOGOPESHA SANA.
 
Safi sana mkuuu na asante kwa ushauri ila nivem urudiii kila baada ya muda kwa vipimooo zaid
 
Back
Top Bottom