CHIPESI NAMISUKU
Member
- Oct 7, 2019
- 51
- 157
1. Vyama vya Upinzani nchini vina nafuu kubwa ya kulelea vijana na kuwafanya kuwa wanasiasa wakubwa mbeleni.
Ni rahisi sana kwa kijana ambaye hana fedha lakini yupo Smart kushinda Ubunge akiwa Upinzani kuliko kwenye chama chetu tawala.
Tuna mifano Halisi kabisa angalia Umri aliopata nao Ubunge Zitto, Kafulila, Nassari, John Mnyika, Felix Mkosamali na wengineo kwenye mlolongo huu. Mkosamali yeye alishinda Ubunge akiwa Chuo kikuu pale SAUT, Kwa CCM si rahisi kihivyo.
Kura za maoni zilizoisha za wagombea Ubunge kwenye majimbo ndani ya CCM tumeshuhudia na kuthibitisha kuwa ni vigumu Sana kwa kijana wa baba na mama mkulima kupenya kwenye tundu hili na kufanikiwa kuwatumikia wananchi.
Ni vigumu, ni vigumu sana, Mfumo ulivyo ni vigumu zaidi. Wengi wanaofanikiwa kupenya account zao zinasoma vizuri na wanakwenda kwenye Utumishi wa Umma na hasa Ubunge kulinda Biashara zao, na kujilinda wao zaidi.
Nina Matumaini makubwa kuwa tabia hii itakomeshwa kwa kuwa tuna Viongozi waadilifu kwenye chama. Mwenyekiti wetu, katibu Mkuu wetu na Mwenezi wetu nikisikiliza kauli zao napata Matumaini makubwa kuwa wanaweza kuondoa Hali hii na kukirudisha chama hiki kwa washika Jembe na Nyundo kwa maana ya wakulima na wafanyakazi.
2. Kuna tetesi kuwa watumishi wa Umma walioshika fomu mwaka huu kugombea wanaweza kukutana na Adhabu Kali. Narudia kusema kuwa Kuna tetesi... Kama ni kweli tutakuwa tumerudi nyuma hatua Mia moja.
Mwalimu Nyerere alitukomboa watanzania toka kwa mkoloni Siasa za ukombozi alizianza akiwa Mwalimu.
Rais tuliyenaye ametokea kazini akaelekea Ikulu akiwa Mwalimu.
Katibu wetu mkuu Dkt. Bashiru ametokea kazini akawa katibu akiwa Mwalimu.
Tukitaja list ya waliotokea kwenye Utumishi wa Umma wakaingia kwenye Siasa hatutamaliza leo.
Je, ni Rasmi Sasa watumishi wa Umma Wote hawaruhusiwi kushiriki Siasa? Hili liwekwe wazi itawasaidia kutokukutana na panga la Mwajiri.
Je, uongozi wa Taifa hili watumishi wa Umma hawaruhusiwi kuutafuta? Ok labda wanapaswa kuwaachia Boda Boda na Wafanya Biashara. Bendera yetu naona bado Kuna jembe na Nyundo... Au wafanyakazi wabakie kuwa wapiga Kura tu au kusimamia chaguzi? Hatuoni tuna Minya Sana uwezekano wa kupata Viongozi Bora?
Katiba yetu inasemaje?
Narudia kusema kuwa Kuna tetesi Kama ni za Uongo Mamlaka zitoe kauli kuwa ni Uongo ili watumishi waliochukua fomu wasibughudhiwe, Kama ni za kweli mamlaka pia zitoe kauli na kufafanua misingi ya Kauli hii.