Baada ya kusambaa video ya msanii maarufu kuathiika na madawa, huu ndio ushauri wangu

Baada ya kusambaa video ya msanii maarufu kuathiika na madawa, huu ndio ushauri wangu

sky soldier

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2020
Posts
5,407
Reaction score
19,264
Kujificha kutumia madawa ni kama kupanda mnazi chooni, huo mnazi utaota kwa kutumia mikojo na mavi kama mbolea, kuna siku utaonekana bila kificho.

Haya madawa aidha uanze kuyatumia mwenyewe, ufundishwe ama kutumia visingizio kwamba ulishinikizwe na marafiki au uliyatumia kuondoa stress, nk yanakufikisha sehemu moja tu ambayo ni kifo, jela ama uteja ulioambatana na upungufu wa akili au afya.

Watu wengi maarufu kama wasanii wakianza kushuka mafajikio wanapata stress sana hasa ukizingatia wanajulikana ma watu wengi,

Uamuzi wa kuanza kutumia madawa kwa kisingizio cha kutoa stress hua ndio mwanzo mbaya wa kuwa teja, kujichimbia kaburi ama kwenda jela.

Nampa big up shilole katumia jina lake kuwa mama ntilie, kaweka usupa staa pembeni, maisha yanaendelea.

Pia nae Lamar fish crab aliekuwa producer wa mziki nae anapika chakula na huwa anawahi asubuhi ufukwenu kununua samaki kwa wavuvi ili anunue kwa bei ndogo kuzidi wakifika sokoni (akili hii sio ubahili), kuna kipindi anvyoanza kupika chakula aliacha kutumia prado yake, aliweka aibu pembeni, hapo kumbuka aliwahi kusoma feza boyz shule ya milioni 6. Kwa sasa mambo yake si haba.
 
Achana nao hawatakusaidia kitu, kwani topic ya madawa ya kulevya hawakuisoma shuleni. Kwani kitabu cha Kilio Chetu hawakukisoma. Acha dawa iwaingie vizuri.
 
Lazima tunyonge, tunuse, tudunge, RUNGWE, ili kutoa stress ushauri tunaopeana, wakati saikolojia inahimiza mazoezi huondoa stress na kuimarisha afya ya akili, sisi tunashauriana madawa balaa sana
 
Back
Top Bottom