Baada ya kutua mwezini, India sasa yaelekea Juani

Webabu

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2010
Posts
8,870
Reaction score
14,258
India ndio nchi ya mwanzo kufanikiwa kutua kwenye ncha ya kusini ya mwezi ambako ndiko kwenye matumaini zaidi ya kuwepo kwa maji yatakayorahisisha kupiga kambi huko kwa ajili ya tafiti zaidi kuhusu ulimwengu.

Baada ya mafanikio hayo wiki kadhaa zilizopita kwa kutumia chombo cha Chandrayaan sasa nchi hiyo imefanikiwa kurusha roketi ya Aditya-L1 inayotarajiwa kufika juani baada ya miezi 4.

Adity itasafiri kilomita 1,500,000 mpaka itakapofikia sehemu ijulikanayo kama Lagrange kwenye uso wa Jua.Nchi kadhaa ikiwemo Japan tayari wameshapeleka vyombo vyao tangu 1981 ili kupata takwimu mbali mbali zinazohusu jua na matokeo yatokanayo nalo.

 
Safi sana, kuna nchi yenyewe inang'ang'ana kuwavua watu ubalozi
 
Wanajitahidi kutudanganya,sijui wanapata faida gani.Uongo nasema Uongo
 
Kumbe wanatuma vyombo🤔,nilidhani wao wamefika huko mwezini na juani.
 
Kumbe wanatuma vyombo🤔,nilidhani wao wamefika huko mwezini na juani.
Hpana.Wanatuma vyombo tu na ni shughuli pevu. Juani hakuna anayepanga kwenda na hiwezekani.
Mwezini tu hakuna aliyefika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…