Baada ya kutua Simba S.C.. Mavugo anena mazito.

sembo

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2011
Posts
4,350
Reaction score
3,451
Mchezaji bora kabisa toka nchini Burundi, aliye daraja moja na kina Messi, CR7 na Suarez [hii ni kutokana na rekodi yake ya kufunga goli 29 katika mechi 28], Laudit Mavugo.. baada ya kusaini mkataba Simba S.C anena mazito.

Namnukuu.. "Sikutaka kusaini pale Vital'O kwavile tu nina deni hapa Simba tangu mwaka jana, nimekuja kulipa. Hawa watu wa Simba ni wavumilivu sana, wangeweza kunishtaki lakini hawakufanya hivyo, waambie watulie nimekuja kuwafanyia kazi."

Ukweli kuhusu zile tetesi za kufeli majaribio nchini Ufaransa.
Mavugo alikwenda katika klabu ya Tours iliyopo nchini Ufaransa kwa lengo la kufanya majaribio.
Lakini alipofika walimtaka akae kwenye 'Academy' yao ili ajifunze zaidi soka la kimataifa kwa mwaka mmoja bila kulipwa mshahara badala ya kufanya majaribio kama alivyoambiwa wakati anaenda.
Jambo hilo lilikuwa gumu kwa straika huyo ndipo alipoamua kuja Simba S.C.
Hii inshu inanikumbusha, lile sakata la Shomari Kapombe.

Laudit Mavugo ambaye atatambulishwa rasmi Simba Day [Agosti 8, 2016] tayari ameshajiunga katika kambi iliyopo Jijini Dar es Salaam.
 
Simba bado sana nafasi ya 3 kwenye vpl inawahusu!
 
Na kweli mnapaswa kutushukru maana wachezaji wengi mlionao tumewalea sisi...mfano namba 1-5 kutoka Simba ni 5 wote kutoka simba
Ndio utani huo na pia wamefuata maslahi nami nimefarijika namna mimi na wewe tunavyojadiliana bila mapovu wala kejeli hii inadhihirisha ukomavu wetu katika michezo kiukweli nimependa mjadala wetu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…