Nimepata bahati ya kusoma vitabu vingi vy Mwandishi mahiri wa Vitabu Bwana Robert Kiyosaki,huyu Bwana ametoa vitabu vingi ambavyo ukivisoma kwa umakini unaweza kupata maarifa mengi sana yanayohusu mambo ya Mifuko hii ya Jamii.Anachotufahamisha ni kuwa Wafanyakazi tukiendelea kuitegemea Mifuko hii ili tunapofikia wakati wa uzee itusaidie tutakuwa tunajidanganya sana! Kwa mifano aliyoitoa hapo Marekani ni kama vile Wafanyakazi wanatapeliwa kwa kuwekewa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ambayo wao kama Wafanyakazi hawana maamuzi nayo na kwa hapa kwetu Tanzania hali ndiyo inazidi kuwa mbaya zaidi,kwa mfano Ujenzi wa Jengo la Bunge fedha zake kwa kiwango kikubwa zimekopwa NSSF na mpaka hivi sasa ulrejeshwaji wa mkopo huo una utata. Jengo la Machinga Complex nalo halijaanza kurejesha fedha kutoka kwenye Mfuko wa Jamii iliyokopa na inaonekana ulipaji wake utakuwa mgumu baada ya Halmashauri ya Manispaa ya Ilala kukiri kuwa Jengo hilo halitumiki kama ilivyokusudiwa hali ambayo inaweka rehani fedha za Wafanyakazi. Pia juzi juzi tu tumeona Raisi akizindua ujenzi wa Daraja la Kigamboni daraja ambalo linajengwa kwa fedha za mkopo kutoka PPF. Kwa kweli hali ya Mifuko hii ya Jamii Kifedha siyo nzuri na ndiyo maana kipindi cha Bunge lililopita Serikali ilileta Mabadiriko ya Sheria ambayo yangewalazimisha Wafanyakazi kusubiri mafao yao bila kulipwa kwa muda mrefu mpaka watakapo timiza kigezo cha umri wa miaka 55 hivyo kusababisha mtafaruku mkubwa. Tujifunze kutoka kwa wenzetu waliokuwa kwenye Mifuko hii kwa muda mrefu na matatizo waliyokutana nayo.Mifuko ya jamii nchini ambayo inachangiwa na wafanyakazi imegeuzwa kuwa chanzo cha kulipia miradi ya serikali badala ya kuhifadhi jamii yaani wanachama wake. inasikitisha kuona kuwa, wanachama hawana maamuzi juu ya mifuko hiyo na kulazimishwa kuchukua fedha hizo baada ya kuzeeka. hii ni dalili tosha mifuko hii imefulia na haina pesa za kutosha: