Tlaatlaah
JF-Expert Member
- May 18, 2023
- 24,665
- 25,388
Washirika wake wa chama chake cha UDA na Muungano wa KENYA KWANZA maseneta, wabunge na magavanor bado wanamuona ni mtu pekee na muhimu zaidi katika kuwaunganisha wa Kenya na kuwaletea maendeleo endelevu katika maeneo yao. Wana Imani nae sana licha ya vijana kutaka ang'atuke mamlakani.
Sambamba nae, kinara wa ODM Raila Amolo Odinga na Muungano wa AZIMIO LA UMOJA-ONE KENYA COALITION nao hivi sasa wanaambatana na Rais William Ruto katika matukio mbalimbali ya kitaifa, majuzi wakijumuika katika hafla ya utiaji saini mabadiliko ya sheria ya tume Huru ya Uchaguzi kenya IEBC, lakini pia jana wakijumuika pamoja huko Kajiado wakati wa uzinduzi wa mtandao wa kusambaza umeme wa Kimuka Power Substation huko Kajiado, mradi ambao utaleta ahuweni na kusogeza huduma za uhakika stima kwa wananchi wengi zaidi katika maeneo hayo na mengine ya jirani.
Ni dhahiri muunganiko wa miungano hii hasimu ya kisiasa itadhoofisha vuguvugu la gen z na kuwagawanya, na hivyo kufanya utawala wa Ruto kuwa rahisi kuchukua udhibiti thabiti wa vuguvugu hilo ambalo lilijizolea umaarufu mkubwa, na lakini kwasasa taratibu likipoteza umaarufu, malengo na uelekeo, huku likijivika sura ya kihalifu.
Rais William Ruto amelaumu, kuyanyooshea kidole na kuyaonya mataifa ya magharibi kufadhili na kuchochea vuguvugu la gen z, kuleta fujo na kusababisha uharibifu na kuvuruga amani Kenya na kwamba Taifa lake na uongozi wake uko makini sana hawatafanikiwa.
Unadhani anazilenga nchi gani hasa za magharibi, kwamba ndio wafadhili wa kuu wa gen z, kupitia mahasimu na watangulizi wake kisiasa?🐒