Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Fortunatus ameyasema hayo alipokuwa akifanya mahojiano maalum na Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Prof. Mohamed Janabi katika kipindi cha AFYA PODCAST ambapo amebainisha kuwa hakuchanwa popote ili kuwekewa puto na ulaji wake umebadilika sana.
Aidha, Prof. Janabi ameihakikishia jamii kuwa huduma hiyo ni salama na inatumia teknolojia ya hali ya juu duniani ambapo dhumuni lake ni kumtengenezea mtu utamaduni wa kula kidogo na kwa kuzingatia mlo kamili kwakuwa puto linakuwa limechukua moja ya tatu ya tumbo na mbili ya tatu inabaki kwa ajili ya chakula.