Baada ya Liverpool kufungwa na kutolewa kwenye UEFA ya msimu 2019/20. Yafahamu haya

Influenza

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2018
Posts
1,509
Reaction score
3,756
Liverpool imetolewa katika Michuano ya Klabu Bingwa Ulaya kufuatia kufungwa goli 3-2 na Atletico Madrid ndani ya dakika 120. Dakika 30 ziliongezwa baada ya dakika 90 kuisha Liverpool ikiwa inaongoza kwa goli 1-0

Jana, kwa mara ya kwanza Liverpool imecheza mechi hadi dakika za nyongeza kwenye Klabu Bingwa Ulaya tangu ilipofanya hivyo mara ya mwisho Aprili 2008 dhidi ya Chelsea kwenye mchezo wa nusu fainali. Liverpool ilitolewa

Liverpool imetolewa kwenye hatua ya 16 Bora mara ya kwanza tangu ilipotolewa na Benifica mwaka 2006. Ilikuwa pia Bingwa Mtetezi baada ya kushinda taji la Klabu Bingwa Ulaya mwaka 2005

Kwa mara ya pili katika historia ya Liverpool, timu hiyo imefunga goli mbili na kutolewa katika michuano ya UEFA, mara ya kwanza ni dhidi ya Udinese mwaka 2012 ilipofungwa goli 2-3 katika michuano ya Europa

Tangu msimu wa mwaka 2017/18, Magolikipa wa Liverpool wamefanya makosa mengi yaliyosababisha kufungwa kuliko magolikipa wa timu yoyote kwenye Klabu Bingwa Ulaya (4 - Adrian x1 + Karius x3)

Marcos Llorente ni mchezaji wa pili wa Atletico kufunga goli mbili katika mchezo mmoja akitokea benchi kwenye michuano hiyo tangu Novemba 2009, Sergio Aguero alipofunga dhidi ya Chelsea
 
Kipa ni muhimu sanaaaa
Kuumia kwa allison kumewacost
Tuombe mungu corona isije kuvuruga na huku
Kulikobakia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…