Baada ya mabwawa ya Libya kupasuka na kuua watu zaidi ya 11,000, je bwawa gani chakavu litafuatia?

Jifunzeni kua na akili, siyo mpaka majanga yatokee nchi zingine ndiyo mnajifanya na ninyi mnaweza kufikiri kumbe ni Bure tu, hiki ulichosema ni sahihi kabisa, lakini ulikua wapi kuishauri serikali

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwahiyo aache tu? Kwani hao sivili injiniaz wanafanya kazi gani kwanini wao wasishauri mapema?
 

Three Gorges Dam,
 
CCM haijengi hilo bwawa. Bwawa linajengwa na wataalamu makampuni ya nje. Hizo nyufa ni za kupumulia pale maji yakizidi kimo.

Punguzeni hasira na CCM. CCM tunaiba kura lakini hatutengenezi mabwawa.
 
Hakuna cha kuomba hapa tumeyataka wenyewe.

Makamba wamemtoa baada ya kuona haya kumwondolea aibu ya karne...

Tunaposema Makamba anabebwa mtuelewe. Hajatumbliwa ila kasafishwa
... ila tukiwa wakweli wa nafsi zetu; Makamaba anahusika vipi na ubovu ulioonekana kwenye bwana? Maskini ya Mungu mkataba uliingiwa hana hili wala lile; ujenzi unaanza hayupo serikalini; kaja kusukumiziwa dakika za mwisho ujenzi wa concrete ni 100% umekamilika! Hata kama ni chuki, this is too much.
 
Hakuna cha kuomba hapa tumeyataka wenyewe.

Makamba wamemtoa baada ya kuona haya kumwondolea aibu ya karne...

Tunaposema Makamba anabebwa mtuelewe. Hajatumbliwa ila kasafishwa
Kwani Makamba ndio mkandarasi wa hilo bwawa!? Halafu wakati akipewa mamlaka siamekuta mradi umeshaanza kutekekelezwa muda mrefu!?
 
Kufa kufaana
 
Ndicho marekani walikitarajia baada ya kifo cha gadafi
 
Bwawa ni jina tu lakini yote ni jengo kanuni zile zile.
Nyumba,guest,frem, ghorofa zote ni kitu kimoja
Ulitakiwa kusema "yote ni majengo" na sio "yote ni jengo". Alafu guest, nyumba,frem sio kitu kimoja
 
Bora hata hayo tunajua yamekaa muda mrefu, je na lile ambalo halijaanza hata kutumika na lina nyufa itakuaje?
Sio bwawa hata hio Barabara ya mwendo kasi bado haijaanza kutumika lkn zege linatoa nyuma inabidi mkandaras anakat wanaweka viraka ni dalili ubora hafifu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…