Baada ya Magufuli, TANESCO wanaanza kata kata ya umeme

mkuu nakutabiria utakufa kifo kibaya sana
 
Ni imani yangu kuwa mifumo imara aliyoiunda kama ipo ndiyo itakayofanya kazi.
 
Ni kweli japo nilimpinga jiwe kwa mambo mengi Sana ,Ila suala la umeme alilidhibiti.Sahivi panya wa tanesco wanatawala.Hata kuja kukufungia umeme wanadai Hamna mita,Jambo ambalo halikuwepo enzi za mwendazake
Acha uzwazwa nadai mita mbili za umeme tangu December. Na pia tangu November wamesitisha kutoa huduma ya Nyongeza ya Luku kwa nyumba iliyo na Luku tayari.
 
Kwakweli JPM alijitahidi Sana kutengeneza mabumunda na zero brains za kutosha including mleta mada, kwamba wakati wa jpm umeme haukukatika! Jitu linabwatuka kwamba umeme ulikuwa haukatiki kisa biti za mwenda zake as if unaowaambia huu utopolo hawakuwepo tz! Shindwa na ulegee kama huyu jamaa aliwalisha limbwata msidhani kwamba wote timeless.
 
Ni kweli japo nilimpinga jiwe kwa mambo mengi Sana ,Ila suala la umeme alilidhibiti.Sahivi panya wa tanesco wanatawala.Hata kuja kukufungia umeme wanadai Hamna mita,Jambo ambalo halikuwepo enzi za mwendazake
Labda kwenu....nilipo mimi umeme ulikuwa unakatwa sana ru...tofauti na sasa.
 
Hizo technical problems ambazo hazikujitokeza kipindi cha JPM ndio zimeanza kujitokeza mara tu baada ya JPM?
Matatizo ya umeme kukatikakatika yalianza toka mwaka jana mwezi wa kumi sijajua tatizo nini hata Rais Samia akiwa Makamu wa Rais alisema kukatikakatika umeme sasa basi maneno hayo aliyasema akiwa ziarani Mkoani Tanga tusipende kupotosha vitu bila sababu yoyote ya msingi
 
Usiwe mchonganishi , karta kada ya TANESCO nimeanza toka JPM anapumua!
 
Usipate taabu watakuja wawekezaji kumaliza tatizo...sasa tumefungua milango kwa wawekezaji
 
Ndugu utaambulia matusi na kashfa hapa, hua nawaza hawa sijui ndo wafuasi wapya wa ...... au sijui ni bavicha sijui hata lengo lao ni nn. Hawataki vitu vya kutumia logic kabisa.
Siku hizi Chadema wapo sambamba na mama na kuna wengine walishatoa matamko kuwa hawatokuja kuipenda Ccm kamwe na mama ni kada mzito ndani ya Ccm sasa unabaki unashangaa na kujiuliza hawa watu vipi
 
Iringa mlifanya makosa sana kukubali Peter Msigwa kuporwa ushindi wake wa ubunge,Msigwa aliidhibiti sana Tanesco,hakuwa anakubali wapiga kura wake wakatiwe umeme.
 
MBEYA nako kila siku umeme unakatwa hapo ndipo namkumbuka JPM
 
Mbona wakati wa jpm umeme ulikua unakatika sema angalau alimudu kiasi. So tusimstress mama
 
Ilikuwa marufuku kukatakata umeme kabla ya 17 Machi? Mbona hakuna aliyetuambia sisi? Mbona mitambo hapa Masaki haikuarifiwa?
Au tulikuwa na tatizo la macho tulipoona giza mara kwa mara (si kwa muda mrefu, lakini mara kwa mara.)?
Mafumbo mafumbo!
 
Julius Nyerere Hydropower Project "MEGA PROJECT"ni ya nini kama hakuna tatizo la umeme..💪🇹🇿👍
 
Duuuu yaan Uhuru wa kutoa kutoa maoni usipodhibitiwa tutasoma mengi Sana ya ajabu kuwahi kutokea katika mitandao hii ya kijamii. Yaani hyu nae ndo kapost bonge la post
 
Ni kweli japo nilimpinga jiwe kwa mambo mengi Sana ,Ila suala la umeme alilidhibiti.Sahivi panya wa tanesco wanatawala.Hata kuja kukufungia umeme wanadai Hamna mita,Jambo ambalo halikuwepo enzi za mwendazake
Kwa mwaka unafunga mita Mara ngapi mkuu?
 
Nina siku nyingi kidogo nje ya JF,kumbe MATAGA mnatia huruma ivi!? Poleni Sana!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…