Pre GE2025 Baada ya Mahojiano na Tundu Lissu mwandishi Sammy Awami apiga hodi nyumbani kwa Freeman Mbowe kwa Mahojiano pia!

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Nimegundua Lissu kwa siasa za one to one bado mchanga sana.

Kadri wanavyozidi kuhojiwa namuona Mwamba akitoka na tuzo huku Lissu anaishia na hoja zake zilezile kwamba aondoke tu sababu katawala miaka 21 atakuwa kama mugame..
Lissu ana 57 na Mbowe ana 61. Yaani Lissu bado anajifanya kijana kumbe ni dingi tu na yeye.
 
Lisu kasema ameifanyia nini chadema kwa miaka yote ya uanachama na uongozi wake? Kijamaa kinajua kupiga porojo hicho !!!
Hivi unajua kuwa hata hiyo ruzuku ya CHADEMA ambayo mnaitafuna ni kutokana na kura alizopata kwenye ule uchaguzi kiinimacho wa 2020?
 
Hivi unajua kuwa hata hiyo ruzuku ya CHADEMA ambayo mnaitafuna ni kutokana na kura alizopata kwenye ule uchaguzi kiinimacho wa 2020?
Post #14 imejibu vizuri sana hii hoja yako.
Btw, mimi sina chama kwa hiyo siyo mtafuna ruzuku!
 
##Waende hivyo hivyo. Ni vyema kuwafahamu viongozi wetu hawa;

➑ Tujue reaction/mwitikio wao wakiwa katika nyakati na majira amani ya mioyo na nafsi zao...

➑ Tujue reaction/mwitikio wao wanapopambana na hali wasizozipenda/wanapohisi wamechokozwa au kuingiliwa...

➑ Tujue reaction/mwitikio wao wanapohisi maslahi yao yameingiliwa...

➑ Kikubwa zaidi tuwajue kupitia kauli zao iwapo ni viongozi kweli walio tayari kuongoza watu wao kwenda kwenye mafanikio na ustawi wao au ni viongozi watafuta kuabudiwa/sifa tu na kutumia taasisi wanaziongoza kujinufaisha wao binafsi na rafiki zao...

## Salimu Kikeke naye aende au afanye utaratibu wa kuhojiana na Tundu Lissu pia ili hoja zilizotolewa na Mbowe wakati akimhoji, Tundu naye ajibu..
 
Wenje: Makamu Mwenyekiti wa Chadema ni Cheo kidogo sana hakunaga majukumu tangible zaidi ya kuongoza Vikao Vya Nidhamu
Kwahiyo Unasema Tundu Lisu anaongoza vikao vya nidhamu CHADEMA?

Na nidhamu yake nanini anaisimamia sasa ndani ya chadema?

Amekuwa akiongea hovyo uongo bila ushahidi wowote, kila siku amekuwa akituambia Mbowe,Wenje na wale asiowapenda ndani ya chadema wamehongwa pesa kutoka kwa Abdul na Mama yake, lakini hajawahi weka ushahidi popote licha ya kusema, vikao vyote vya Abdul na hao wala rushwa vilikuwa recorded kikiwemo kikao chake yeye na Abdul na wenje walipomfuata kumpa rushwa, anayodai aliikata.

Nashindwa kuelewa ikiwa yeye ndiye anasimammia nidhamu na nimwanasheria, alipaswa kutupa ushahidi hata kam sio wote basi vionjo ili tuwe na imani wakati akiuandaa kuwasilisha kwenye kamati kuu ya chama, Balaza kuu na hata TAKUKURU kama utahitajika ili kuwashughulikia watoaji na wapokeaji?
 
Akitoka kwa Mbowe arudi kwa Lissu ili ajibu hoja za Mbowe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…