Mpiga gitaa maarufu wa Kongo Denis Lokassa Kasiya, almaarufu Lokassa ya Mbongo, alifariki Jumanne usiku nchini Marekani baada ya kuugua kwa muda mrefu. Lokassa, ambaye hivi majuzi alifikisha umri wa miaka 80, alikuwa kiongozi wa bendi maarufu ya zamani ya Soukous Stars yenye makao yake Paris...