Baada ya makato ya simu sasa ni bei ya Mbolea

Baada ya makato ya simu sasa ni bei ya Mbolea

kidadari

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2012
Posts
8,647
Reaction score
9,604
Wakati wananchi wakipaza sauti kulalamikia tozo za miamala ya simu ambayo imeonekana kua mzigo na maumivu kwa wananchi sasa bei ya mbolea imeenda kupaa isivyo kawaida hivyo kuketa taharuki wa wakulima.

Kilimo ndo uti wa Mgongo wa taifa ambapo zaidi ya 70% ya wananchi wanajishughulisha na kilimo.

Bei ya mbolea imepanda gafla zaidi ya 30% jambo lisilo la kawaida ambapo mbolea ya urea iliyokua inauzwa 56,000 sasa imefika 84,000 . Huku Yara, DAP na CAN ikifika 86,000.

Tusuburi maumivu kwa wengi maana hiki kitakua kilio cha pili baada ya Makato ya miamala simu.
 
Mbolea zimepanda maradufu... Mwaka ulopita wakiserikari ktk budget mfano mbolea ya primium DAP njombe ilikuwa 64,000/ Leo hii tawi lao primium njombe wanauza 88,000/ kwa mfuko wa 50kg.. Mbaya zaidi waziri mwenye dhamana amewapongeza wanao uza 80,000 maana ametoa ushuhuda kuwa dar ni 85,000/=
 
Safi Sana,kueni wazalendo tumieni samadi.

Nasema uongo ndg zanguuuuuuuuuu.
 
Halafu mkulima anaishia kuuza bei ya hasara, kwa sasa ndo wakati wakulima kupitia vikundi vyenu muweze kujenga maghala ya kuhifadhi mazao yenu muuze kipindi bei imechangamka na hata uwezekano wa kujenga viwanda vya kuchakata mazao yenu, kuongeza thamani na ubora. Serikali ndo imeshawatosa hivyo.
 
Halafu mkulima anaishia kuuza bei ya hasara, kwa sasa ndo wakati wakulima kupitia vikundi vyenu muweze kujenga maghala ya kuhifadhi mazao yenu muuze kipindi bei imechangamka na hata uwezekano wa kujenga viwanda vya kuchakata mazao yenu, kuongeza thamani na ubora.....serikali ndo imeshawatosa hivyo...
Wanaweza wanafanya hivyo na wakapewa kesi ya uhujumu uchumi.
 
Acheni kelele nyie, hayo ni maumivu ya muda mfupi, mama atafungulia hela mtaani🤸‍♂️🐒🤣
 
Halafu waziri anakuja na porojo ohhho kutokana na corona , demand imekuwa kubwa sana hatuna uwezo wa kushusha bei!!kwani nini maana ya RUZUKU?serikali makini utasikia wanatoa ruzuku kwenye mambo kama haya yenye mchango mkubwa kwenye uchumi wanashindwa nini kuwasaidia?!!halafu juzi nasikia eti serikali ina angaalia jinsi ya kuvipa vyombo vya habari bail out, kutokana na kuyumba kwao!!hii nchi bwana, mkulima atapambana kivyake akivuna tu wamefika kupanga bei , na kuuza nje lazima upate kibali maalum!!
 
Hili la mbolea limeniuma sana. Mkoa nliopo Urea ni 80K halafu unaambiwa ulime kwa njia za kisasa. Nchi imekua ngumu hii sijui tutaponea wapi
 
Wakati wananchi wakipaza sauti kulalamikia tozo za miamala ya simu ambayo imeonekana kua mzigo na maumivu kwa wananchi sasa bei ya mbolea imeenda kupaa isivyo kawaida hivyo kuketa taharuki wa wakulima.

Kilimo ndo uti wa Mgongo wa taifa ambapo zaidi ya 70% ya wananchi wanajishughulisha na kilimo.

Bei ya mbolea imepanda gafla zaidi ya 30% jambo lisilo la kawaida ambapo mbolea ya urea iliyokua inauzwa 56,000 sasa imefika 84,000 . Huku Yara na CAN ikifika 86,000.

Tusuburi maumivu kwka wengi maana hiki kitakua kilio cha pilibaada ya Makato ya simu.
Duuu, na bado leseni za wavuta sigara
 
Back
Top Bottom