Baada ya Mechi ya simba Vs al ahaly, Simba itacheza fainali msimu wa 2020/2021

Baada ya Mechi ya simba Vs al ahaly, Simba itacheza fainali msimu wa 2020/2021

Ladder 49

JF-Expert Member
Joined
Dec 19, 2017
Posts
7,918
Reaction score
20,037
Wakuu Habari zenu,

Kwa wale ambao mmezoea kukalili zama zimebadilika sana,mbadilike simba hii iko vizuri sana tofauti sana na simba za miaka ya nyuma.

Mechi ya simba na as vita kule Congo ilikuwa inakupa Picha simba ya msimu huu,sio kwamba as vita hawakuwa vizuri bali simba sc walikuwa Hodari kwenye kukaba sana na kutibua mipango ya as vita.

Mwanzo hadi mwisho wa mchezo,bila kupoteza umakini ambao siku zote timu zinakuwa hazina hicho kitu,wanazuia mwanzo mwisho wanafungwa yaani pressure inakuwa kubwa wanashindwa kuhimili.lakini kwa simba ya sasa kwenye klabu bingwa Africa Wanazuia mwanzo mwisho bila kupoteza umakini.

Timu yoyote ikiwa na ukuta kwamba wachezaji wote wanakaba sana mwanzo mwisho kufungwa kwenye mechi ni ngumu sana na ndio nachokiona kwa simba kwa sasa wanakaba sana yaani wamechangamka yaani wanautaka ubingwa wa Africa.

Mechi ya Leo dhidi ya al ahaly,inatosha kabisa kuondoa wasiwasi wako kwa simba sc kwenye kucheza fainali ya klabu bingwa Africa.

Al ahaly imetoka kucheza klabu bingwa dunia na imeshika nafasi ya 3 kidunia aijapita mwezi kikosi kile kile kinafungwa na simba sc ,na kupata shot on target 1 ndani ya dak 90,sio swala dogo.hii simba itacheza fainali.

Adjustments.jpg


Adjustments.jpg



Msimu wa 2018/2019 al ahaly walivyofungwa na simba kwa mkapa nikasema kwasababu al ahaly hakuwa bingwa kwenye hilo kombe ,hivyo hakuwa vizuri lakini msimu huu al ahaly ndio bingwa mtetezi.mechi nzima anapata shot on target moja tu.

Jinsi wanavyocheza msimu huu simba kwenye champions league lazima watafika fainali kama sio kuchukua kabisa.

Mimi simba hii naiona mbali sana msimu huu.

Sidhani kama kuna mtu anawatiliashaka simba kwenye kuvuka kwenye makundi.Leo dhidi ya al ahly ukiambiwa utaje man of the match kila mtu mtu atasema wake kwanini? Kwasababu kila mtu alikuwa anapambana uwanjani, sasa kwa uchezaji huu sasa hakuna wakuwazuia.

Simba itacheza fainali klabu bingwa Africa msimu wa 2020/2021.ni swala tu la muda.
 
Well said ndg. Ladder 49
Uongozi bora na makini ndiyo mpango mzima.
HONGERA wanaMsimbazi na TAIFA kwa jumla.

Timu/clubs na TAASISI zingine tuepuke ujanjaujanja na masilahi binafsi.... !!
Simba ilijiandaa muda mrefu sana kwenye hayo mashindano hilo liko wazi kinachoonekana hapo Leo sio bahati.
 
Yani game moja tayari mmeshaanza kelele?tujipe muda tutarudi tena kwenye huu uzi.
 
Jamaa unafatilia mpira kweli?
Yani game moja tayari mmeshaanza kelele?tujipe muda tutarudi tena kwenye huu uzi.
Simba kaanza na mechi mbili nzito na vigogo wa Africa zenye uhakika wa kufika nusu mpaka fainali kila mwaka na zimefungwa.
As Vita ishawaikuchukua ubingwa.

Al Ahly ndo wenye kombe lao mpaka sasa na ni timu bora kwa kilakitu kwa Africa,na ni klabu bora iliyoshika nafasi ya tatu Duniani.
Wewe unaona kazindogo, eti ni mechi moja tu?
 
Back
Top Bottom