OKW BOBAN SUNZU
Platinum Member
- Aug 24, 2011
- 53,868
- 121,001
Hii tathmini nimeifanya kwa muda mrefu sana, takribani miaka 20 sasa. Nimejiridhisha kabisa baada ya miziki ya dini basi mziki unaofuata ni Hip Hop.
Hip Hop ni jina lenye maana kubwa, pana na muhimu zaidi kama mtu utalifuatilia kiundani zaidi. Mfano Manju Kool Herc alisema, "Hip Hop ni kemia (chemistry) iliyotoka Jamaika na kuangaza Dunia nzima".
Lakini swali la msingi ni kujiuliza kwanini Hip Hop ni utamaduni?
• Ni utamaduni kwasababu ni mtindo huru usiyo na ubaguzi na wenye utaratibu maalumu wa kimaisha. Utamaduni huu hauna itikadi za kidini, kikabila, rangi, lugha wala Taifa.
Hapa tunajifunza kuwa watu wenye kutengeneza uhuru kwa kila mmoja wetu pasipo kujali imani wala kasoro zetu. Utamaduni wa hip hop unamruhusu mtu yeyote kujiunga pasipo kujali itikadi yake (pana somo kubwa sana kwetu pia hapa).
Hip hop inajengwa na nguzo kadhaa. Kwa kuanzia nitagusia nguzo moja ya maarifa/ufahamu (knowledge). ili kujiunga na Utamaduni huu ni lazima uzingatie ufahamu ama maarifa utakayoyatoa kwa jamii.
✍Lakini zaidi, naomba tujifunze katika malengo makuu ya utamaduni huu ambayo ni;
1. Kukuza na kuendeleza harakati za ukombozi wa raia katika nyanja zote kama vile uchumi, siasa, jinsia na fikra.
2. Kuelezea, kutunza na kutangaza uhalisia hasa maisha halisi ya mwanadamu. Hivyo humkumbusha mwanadamu maisha yake halisi.
3. Kueneza na kukuza sanaa. Utamaduni huu hueneza na kukuza sanaa kupitia tanzu zake kama fasihi, uchoraji na muziki.