Baada ya Nape, Makamba who's next, Bashe?

Rabbon

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2022
Posts
21,625
Reaction score
33,688
Salaam, Shalom!!

Utulivu kiasi umeendelea kutamalaki mioyoni mwa Watanzania wenzangu baada ya kuondoshwa Kwa waliokuwa mawaziri vijana wa Makamo / Wazee wachanga, Nape Nnauye na January Makamba.

Hivi sasa, amebaki mmoja au wawili watatu kuelekea u haguzi mkuu, Leo tumwongelee mmoja,

Ndugu Bashe baada ya sakata la sukari kutikisa Nchi na kesi zikiwa mahakamani, paliibuka taharuki baada ya Mwekezaji mmoja kudai kuwa mahindi yetu ndani ya nchi anayaongezea madini Fulani fulani, na umma wa wananchi kupinga Kwa nguvu,

Jana tunaarifiwa na Waziri huyu huyu kuwa, Serikali yetu imeridhia matumizi ya GMO kwenye KILIMO chetu, na wanafanya Utafiti Ili kuziruhusu.

Kwamba GMO, yaani mbegu za kupandikiza zisizo halisi, ziruhusiwe kuingia na kutumika nchini tukiwa chini ya waziri huyu huyu Bashe.

Nchi yetu imejitajidi kutunza mbegu zetu za asili kuhakikisha AFYA za wananchi wake zinakuwa salama Kwa miaka mingi sasa, huu ujio wa GMO katika KILIMO chetu, ni threat Kwa AFYA zetu Watanzania, na kwanini mambo hasi yanaendelea kujitokeza chini ya waziri huyu wa kilimo Bashe?

Nikisema waziri Bashe anampa Rais wetu ushauri usio sahihi kuhusu madhara ya GMO Kwa AFYA za Watanzania nitakuwa sijakosea,

Ni ipi Hasa agenda iliyo nyuma ya Waziri huyu?

Je, baada ya Nape na Makamba, nani anafuata kutumbuliwa?

Magufuli,Tanzania tunakukumbuka sana!!

Mungu ibariki Nchi yangu nzuri niipendayo TANZANIA 🇹🇿.

Karibuni 🙏
 
Salaam, Shalom!!

Utulivu kiasi umeendelea kutamalaki mioyoni mwa Watanzania wenzangu baada ya kuondoshwa Kwa waliokuwa mawaziri vijana wa Makamo Nape Nnauye na Yusuph Makamba.

Hivi sasa, amebaki mmoja au wawili watatu kuelekea u haguzi mkuu, Leo tumwongelee mmoja,

Ndugu Bashe baada ya sakata la sukari kutikisa Nchi na kesi zikiwa mahakamani, paliibuka taharuki baada ya Mwekezaji mmoja kudai kuwa mahindi yetu ndani ya nchi anayaongezea madini Fulani fulani, na umma wa wananchi kupinga Kwa nguvu,

Jana tunaarifiwa na Waziri huyu huyu kuwa, Serikali yetu imeridhia matumizi ya GMO kwenye KILIMO chetu, na wanafanya Utafiti Ili kuziruhusu.

Kwamba GMO, yaani mbegu za kupandikiza zisizo halisi, ziruhusiwe kuingia na kutumika nchini tukiwa chini ya waziri huyu huyu Bashe.

Nchi yetu imejitajidi kutunza mbegu zetu za asili kuhakikisha AFYA za wananchi wake zinakuwa salama Kwa miaka mingi sasa, huu ujio wa GMO katika KILIMO chetu, ni threat Kwa AFYA zetu Watanzania, na kwanini mambo hasi yanaendelea kujitokeza chini ya waziri huyu wa kilimo Bashe?

Nikisema waziri Bashe anampa Rais wetu ushauri usio sahihi kuhusu madhara ya GMO Kwa AFYA za Watanzania nitakuwa sijakosea,

Ni ipi Hasa agenda iliyo nyuma ya Waziri huyu?

Je, baada ya Nape na Makamba, nani anafuata kutumbuliwa?

Magufuli,Tanzania tunakukumbuka sana!!

Mungu ibariki Nchi yangu nzuri niipendayo TANZANIA 🇹🇿.

Karibuni 🙏
Wamle kichwa tuu analeta mazoea kazini 😆
 
Back
Top Bottom