Hehehe!! Hapa povu zitatiririka lakini kichapo ni kile kile, ukweli ni ule ule, mtameza au mteme, mfumbe macho au muyafungue, lakini kinara wa EAC na Kati ni Kenya.
Hadi muunganishe bajeti za nchi zote za EAC ndio mnusie ya Kenya. Hii tofauti inaendelea kuwa kubwa, hapo awali haikua hivi, haswa miaka ya themanini, lakini baada ya Wakenya kubadilisha utawala dhalimu, mambo yakawa mwendo kasi. Halafu ndio mtakoma maana mipango iliyopo kwenye miaka mitano ijayo, Kenya itatoweka kabisa maana hatuna ligi humu EAC.
Sasa hivi tunawaza jinsi ya kuwalisha vumbi majitu kama Nigeria.
Cha msingi tumehakikisha elimu elimu elimu ndio muhimu Kenya, na nguvu kazi yenye kujituma.
Labda muombe sana, ikiwezekana hadi mpige ramli tuingie kwenye machafuko 2017, muwaunganishe waganga wote kwenu na wachawi muwapeleke msituni wakafanye yao dhidi yetu usiku na mchana, vinginevyo mtazidi kuisoma namba. Na hata 2007 tuliingia kwenye vurugu na bado hamkunisia hata makalio yetu, tumechezea mabomu ya alshabaab lakini bado mnaisoma namba.
Bajeti yenu ndogo lakini bado mnategemea misaada na madeni, hata kwa kabajeti kadogo nusu ya Kenya bado mnatembeza kibakuli na kopo la msaada, halafu hamna aibu kuleta mada eti Mbeya vs Eldoret.