Ni kweli nyuzi kama hizi huwa hata sizifungui, mkamate ng'ombe mara ngamia, mchome vifaranga na sijui vitu gani hivyo kisha mje kutambia humu halafu utegemee niseme nini, binafsi nilishawazoea mlivyo majitu yaliyojichokea kwa chuki, wivu, uzembe na umaskini uliokubuhu ile siku mlikamata wamama wa Kimaasai kutokea Kenya wamekutana vikoba na wamama wa Kimaasai wa Tanzania tena huko huko wilaya ya mpakani ambapo kunaishi wamaasai, kabila ambalo pande zote mbili wameishi kama ndugu hata baada ya kufanyiwa unyama na mzungu wa kuwagawa kwa misingi ya kuwachorea mpaka, sasa mkoloni mweusi ndiye anapambana kuwagawa kabisa na kupandikiza chuki baina yao.
Tangu hilo la hao wamama wa Kimaasai, ni wazi hamuwezi kuendana na jirani yeyote mlishavurugwa, itabidi muachwe kama mlivyo, sema mama Suluhu anajaribu kurekebisha lakini atajichokea sana mama, kwanza wenyewe ndani huko mlishaanza kumchosha na vibweka vyenu.