BigTall
JF-Expert Member
- Mar 9, 2022
- 525
- 1,257
Ujenzi ukiendelea
Kama hukuona andiko langu la awali, lipo hapa ~ Hali ilivyo Shule ya Msingi Kamama (Tabora) inasikitisha, vyoo ni chakavu na vichafu, madarasa ndio usiseme
Nimepita mitaa hiyo na kushuhudia ujenzi wa Vyoo ukiendelea kwa kasi eneo hilo la Shule hiyo, nilipouliza mmoja wa mafundi wanaoshiriki ujenzi huo akaniambia kuwa mipango iliyopo ni kujenga hadi madarasa ambayo nayo yanaonekana kuwa chakavu.
Kiukweli vile vyoo ambavyo bado havijabomolewa ni tishio kwa watumiaji, ni chakavu sana kama ilivyo madarasa.
Tusisubiri majanga yatokee kisha ndio tuanze kusema ningejua ningefanya hivi au vile.
================ =================
MAJIBU YA VIONGOZI
Jamii Forums ilipowasiliana na Mkuu wa Wilaya ya Uyui, Zakaria Mwansasu pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Paul Chacha kwa nyakati tofauti na kuwauliza kuhusu shule hiyo na kuhusu hoja ya Mdau, haya ndio yalikuwa majibu yao:
DC WA UYUI, Zakaria Mwansasu :
Utaratibu wa kuripoti jambo unakuwaje? Huyu Mwananchi aliyeripoti kwenu si anaijua Ofisi ya Mkuu wa Wilaya na ya Mkoa zilipo, Mwananchi anatakiwa abalansi huku na huku kisha ndio aandike taarifa yake, nakushukuru (akakata simu).
MKUU WA MKOA, Paul Chacha:
Ungekuwa wewe ungejibuje? Mimi sijui sijaona hiyo taarifa unayoniuliza, wala sina taarifa kuhusu Shule ya Msingi Kamama, sina taarifa unataka nikuambiaje, mimi sijui unachokisema na siwezi kukujibu chochote.
VYOO VYA AWALI
Pia soma:
~ Miundombinu ya Shule ya Msingi Kamama yaboreshwa, Vyoo na madarasa vyajengwa