Pdidy
JF-Expert Member
- Nov 22, 2007
- 57,951
- 32,619
Mwigizaji kutokea nchini Marekani, Leonardo DiCaprio ameamua kujitenga na kujiweka mbali na na Sean 'Diddy' Combs kufuatia kuibuka kwa picha inayoonyesha yeye akiwa kwenye moja ya sherehe maarufu za "white party" zilizokuwa zinaandaliwa na P Diddy.
Kwa mujibu wa chanzo cha karibu na mwigizaji huyo, DiCaprio, mwenye umri wa miaka 49, hajawasiliana na msanii P Diddy kwa miaka kadhaa sasa.
Wiki iliyopita, polisi walimkamata P Diddy, mwenye umri wa miaka 54, kwa mashitaka ya kuhujumu uchumi, biashara ya ngono, na kusafirisha watu kwa lengo la kuwatumikisha katika ukahaba.
Rapa huyo anakabiliwa na tuhuma za kulazimisha wanawake kushiriki kwenye “freak offs,” ambazo ni “maonyesho ya ngono yaliyopangwa kwa ustadi.”
Akizungumza na Daily Mail, chanzo cha karibu na mwigizaji huyo maarufu kilisisitiza kuwa DiCaprio hana uhusiano wowote na kesi ya Diddy na hajawahi kushiriki kwenye “freak offs.” Chanzo hicho kiliongeza kuwa mwigizaji huyo hajawasiliana na rapa huyo aliyekumbwa na kashfa hiyo kwa miaka mingi.
Soma pia: Babu Tale: P Diddy alituita chumbani kwake tukaangalie runinga, Swizz Beatz akatukataza na tukaondoka bila kuaga
"Leonardo DiCaprio hana kabisa uhusiano na lolote kati ya haya," chanzo hicho kilisisitiza kuwa DiCaprio aliwahi kuhudhuria sherehe chache za Diddy mwanzoni mwa miaka ya 2000 kama ilivyokuwa kwa watu maarufu wengine na kwamba sherehe ambazo alihudhuria DiCaprio hazikuwa ni "freak offs."
Source: Daily Mail, Hindustan Times