[Sio kuleta fikira za jaha, eleza ni sifa zipi alizonazo zinazokufanya umkubali kufaa kuwa rais. Mambo ya kusema 'moyo wangu tu unampenda' hayawezi kukubalika. Mimi nampenda Peter Kayanza Pinda kutokana na sifa zifuatazo: Aliweza kuongoza wizara ya serikali za Mitaa na Tawala za mikoa katika kipindi cha wamu ya Tatu. Boss wake wa awamu ya Tatu alidelegate kazi. His hands were off, his eyes on. Huyu Boss wake wa sasa mswahili, anasema hiki anafanya kile. Hajiamini. Anafanya kazi ya kuviziana na hataki mawazo tofauti. Hamtaki mtu anayeweza kum overshine. Ni kiongozi mwenye huruma kwa wanyonge. Kitendo cha kutoa machozi mbele ya Bunge ni in depth feeling kwa wahanga wa mauji ya kikatili ya Albino. Hata Rais Bill Clinton alimwaga machozi uwanja wa ndege alipokuwa akipokea maiti za Wamarekani waliouwawa kwenye mashabulizi ya balozi za Marekani Dar es Salaam na Nairobi mwaka 1998. Viongozi wasioweza kuonyesha hisia za uchungu hata watu wakifa sio majasiri bali wana mioyo ya kikatili. Hisia za huruma au za kikatili hazifichiki. Pinda ni mkweli. Aliposema 'Zanzibar sio nchi' alisema kile kinachoelezwa kwenye Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kwa maneno mengine alikuwa anailinda Katiba aliyoapa kuilinda mbele ya Raisi aliyemteua. Jambo hili JK ameshindwa kutekeleza. Pinda ni shupavu kuliko JK mara 100.QUOTE=Tume ya Katiba;10485355]Subiri ndugu yangu utaona, Membe ana sifa zote za kuwa rais na ndiye anayetufaa kwa sasa.[/QUOTE]