Baada ya Richmond je, bandari ya Dar es Salaam itafuata?

Baada ya Richmond je, bandari ya Dar es Salaam itafuata?

Joined
Nov 5, 2021
Posts
40
Reaction score
24
Nazir Karamagi na Yogesh Manek watafanikiwa kuendelea kuinyonya Tanzania kupitia bandari ya DSM?

Na Juma Kambi, Kuli Bandarini DSM

Wawili hawa ni wamiliki wa kampuni ya kusimamia makontena katika bandari ya Dar (TICTS).Kwa miaka mingi wamekuwa wakipokea mabilioni ya fedha huku utendaji wa kampuni hiyo na bandari kwa ujumla ukisuasua na kusababisha wateja wengi kuhamia Mombasa Kenya, wakikosesha nchi mabilioni ya mapato huku wao wakinufaika.

Manek ni mfanyabiashara nyingi kubwa nchini ikiwemo Benki ya Exim huku Karamagi akiwa Waziri wa zamani wa Nishati na Madini mwenye kashfa ya kusaini mkataba wa madini wa Tanzania mwaka 2007 hotelini Jijini London na mmoja ya wanufaika katika kashfa ya Richmond.

Chini ya utawala wa hayati Rais Magufuli ikafanyika jitihada ya kuanza kuwaondoa na kuboresha utendaji wa bandari, baada ya Magufuli kufariki Rais Samia akaendeleza jitihada hizo. Hivi sasa wawili hao wamejipanga kupambana na Rais Samia ili wapate mkataba mpya kuendelea kubaki bandarini hapo.Swali ni kwamba je watafanikiwa.? Ni suala la kusubiri kuona.

Soma
 
Acha Chuki na watu
Watu wamewekza mapesa ww unaleta ujinga JF
Tafuta hela na ww uwekeze
 
Nazir Karamagi na Yogesh Manek watafanikiwa kuendelea kuinyonya Tanzania kupitia bandari ya DSM?

Na Juma Kambi, Kuli Bandarini DSM

Wawili hawa ni wamiliki wa kampuni ya kusimamia makontena katika bandari ya Dar (TICTS).Kwa miaka mingi wamekuwa wakipokea mabilioni ya fedha huku utendaji wa kampuni hiyo na bandari kwa ujumla ukisuasua na kusababisha wateja wengi kuhamia Mombasa Kenya, wakikosesha nchi mabilioni ya mapato huku wao wakinufaika.Manek ni mfanyabiashara nyingi kubwa nchini ikiwemo Benki ya Exim huku Karamagi akiwa Waziri wa zamani wa Nishati na Madini mwenye kashfa ya kusaini mkataba wa madini wa Tanzania mwaka 2007 hotelini Jijini London na mmoja ya wanufaika katika kashfa ya Richmond.

Chini ya utawala wa hayati Rais Magufuli ikafanyika jitihada ya kuanza kuwaondoa na kuboresha utendaji wa bandari, baada ya Magufuli kufariki Rais Samia akaendeleza jitihada hizo. Hivi sasa wawili hao wamejipanga kupambana na Rais Samia ili wapate mkataba mpya kuendelea kubaki bandarini hapo.Swali ni kwamba je watafanikiwa.? Ni suala la kusubiri kuona.
Hakuna wa kuwazuia MKATABA WATAPATA TU
 
Back
Top Bottom