Baada ya serikali kupunguza bei ya kuunganishiwa umeme kuwa Tsh 27,000 Mkoa wa Kilimanjaro ofisi ya Tanesco mkoa yakabiliwa na upungufu " Surveyor"

'surveyor' hakuwahi kuwa rahisi kupatikana hata kipindi cha 321k

hongo ilihusika ili aje 'fasta' au kwenda branchini kupiga 'kelele'
 
Hawa mameneja wa Tanesco mikoani na wilayani ndiyo wanatengeneza hayo mazingira kwakuwa na wao wanapata gawio humo, mimi nadhani Tanesco HQ watengeneze mfumo ambao wateja watatuma maombi moja kwa moja kwenye mfumo huo, halafu mameneja wa mikoa wapewe maagizo tokea juu, na kila siku jioni utendaji wao upimwe kutokana na idadi ya wateja watakaokuwa wamehudumiwa

Vinginevyo kila jambo jipya la serikali ni fursa kwa wahuni
 
Zaidi ya mwaka wamepanda nguzo zao hapa mtaani kisha wamekuja na swaga za transformer, wakati mita 200+ kuna wadau wanaingiziwa umeme kwa transformer hiyo hiyo wanayodai haitakidhi hadi kwetu, tumeaachia mradi wao hadi wakipata wazo waje, hawataki waendelee kubaki tu, hakuna wa kutoa hela kizembe, nimegoma kabisa
 
Waziri au MD wekeni kwenye jamii forum na vyombo vya habari hii 27,000 imekaaje .lakini naona wako kimya tu.
 
 
Waziri njoo na majibu wananchi huku wahudumiwe kwa matamko yako uli iyotoa.kazi za kuunganisha wateja wapya zimekwama kusubiri maelekezo ya kuunganisha kwa 27,000 kwa kila kaya.ni mwezi sasa karibu tangu watendaji wako wanasubiri ufafanuzi.kwanihyo maana yake ni mwezi sasa tanesco wamekwama kuunganishia wateja wapya.wapunguzieni lawama watendaji wenu kwa watu kwani wao ndiyo wako karibu na wananchi
 
Ninaomba kuuliza, surveyor walioajiriwa na tanesco wanaotakiwa wawe na sifa gani kielimu na wanasomea wapi hiyo kozi? Isije ikawa ni kama traffic polisi kubadilishiwa mavazi . Hiki kitengo ni Cha kuangaliwa kwa jicho la tatu. Kinainyima tanesco mapato makubwa sana kwa uzembe,usumbufu,na Rushwa zao.
 
Wale ni vishoka tu Mkuu wanapewa futi kamba na mameneja wanapima wanagana rushwa maisha yanakwenda mbele
 
Surveyor ni fundi umeme tu, ila hizo ni idara tu, lakini mtu yoyote mwenye ujuzi wa umeme anaweza kufanya kazi ya survey.Tatizo ni hata hao mafundi umeme huko tanesco ni wachache sana.
 
Hata mimi ni muhanga wa hili swala
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…