GRAMAA
JF-Expert Member
- Nov 1, 2014
- 1,241
- 3,800
Mapenzi bwana yanamambo ya ajabu sana.
Ndani ya Mangesani, Bagamoyo kumetokea tukio la kimapenzi la ajabu sana na la kuhuzunisha sana na limewafanya watu wengi washikwe na duwaa.
Tukio lenyewe ni kama ifuatavyo: Baada ya maisha magumu katika familia ya bwana Ismail (mume wa bi Aysha) aliamua kumshauri mke waende kwa mganga ili wakasake pesa ili na wao watusue raha za dunia kama wengine maana walichoka kuishi maisha ya dhiki na umasikini uliopitiliza.
Bi. Aysha mwanzo aligomagoma ili kutokana na ushawishi mkubwa wa mume wake,bi Aysha alijikuta anakubari kwenda kwa mganga na mume wake. Hivyo wakaongozana wote mpaka kwa mganga huko Kigoma.
Walipofika kwa mganga:
Mganga aliwapa huduma waliyokuwa wanataka na mganga alimpa dawa bwana Ismail ambayo ilibidi anywe na akisha kunywa dawa hiyo atakufa kwa muda wa siku saba na mke wake alipewa masharti ya kutokulia ila alipaswa afagie funza tu watakaokuwa wanatoka kwenye mwili wa mume wake ambaye ataoza ndani ya siku saba na baadaye atafufuka na kurudi katika hali yake ya kawaida.
Ila mganga alimwambia bi Aysha kwamba akilia tu basi mume wake atakufa moja kwa moja ila akiweza kuvumilia na kujikaza na kutokulia na kufagia funza zitakazokuwa zinatoka kwa mumewe vizuri basi mumewe akishituka kutoka kwenye kifo hicho watatusua na watapata pesa ndefu sana.
Baada ya mume kunywa dawa:
Ni kweli baada ya mume kunywa dawa alizima kabisa kama mtu aliyekufa. Bi Aysha akavumilia na kujikaza.
Lakini ilipofika siku ya tatu bwana Ismail akaanza kunuka na funza wengi wakawa wanatoka kwenye mwili wa bwana Ismail. Bi Aysha alipoona hivyo akapoteza matumaini kabisa na akahisi mumewe hawezi kuamka tena.
Basi bi Aysha akaanza kulia na kupiga kelele huku akiwaita majilani waje wamsaidie. Majilani wakajaa ila walishangaa kukuta bwana Ismail ameoza vibaya sana hivyo bi Aysha akawekwa chini ya ulinzi na mazishi yakafanywa haraka haraka ya kumzika bwana Ismail.
Alipokuwa kwenye vyombo vya ulinzi bi Aysha ndiyo alisimulia haya yote.
Usimwamini mtu yoyote utakuja kufa kindezi kama bwana Ismail.