Cannabis
JF-Expert Member
- Jan 20, 2014
- 11,557
- 33,535
Tarehe 11/06/2020 Ubalozi wa Marekani umetoa tamko lingine linaloelezea ongezeko la maambukizi ya ugonjwa wa COVID-19 nchini Tanzania, na kuwashauri raia wake kukaa ndani na kuachana na mizunguko isiyo ya lazima. Taarifa hii inafuatia tahadhari mbali mbali ambazo imekuwa ikizitoa tangu ugonjwa huu kufika nchini Tanzania ambazo zilipelekea kaimu balozi wa Marekani nchini Tanzania kuitwa na serikali ya Tanzania na kufanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje. Serikali ya Tanzania ilieleza kusikitishwa na namna Ubalozi wa Marekani umekuwa ukitoa taarifa ya hali ya maambukizi ya ugonjwa huo zisizo sahihi zinazoweza kuzua taharuki kwa Watanzania na wageni kutoka nje ya nchi. Pia serikali ilimtaka kaimu balozi wa Marekani kutoa taarifa zilizothibitishwa na kuwa hakuna kizuizi serikalini kwa mabalozi kupata "taarifa sahihi na zenye ukweli."
Baada ya taarifa hiyo kwa mara mbili mfululizo Ubalozi wa Marekani umeendelea kutoa taarifa zinazokinzana na kauli ya serikali, Rais amehakikishia wananchi wake kuwa ugonjwa umepungua sana na kuwasifu watu wengi anaokutana nao kwa kutokuvaa barakoa, ikiwa ni kielelezo kuwa hali ya hatari ya maambukizi imepungua na inaelekea kuisha Tanzania. Wakati huo huo ubalozi wa Marekani umekuwa ukielezea kuwa kuna uwezekano mkubwa wa kupata ugonjwa huo hatari na kuwasihi raia wake kusalia ndani ama kuondoka nchini Tanzania mara moja pale usafiri wa ndege utakapopatikana.
Vile vile Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania umesema kuwa wakati wowote mlipuko utakapozidi hospitali zetu zitazidiwa na hivyo kuna uwezekano wa Raia wake kukosa huduma kutoka vituo vya afya, lakini Waziri wa Afya amenukuliwa akiwa Dodoma na kusema kuwa hakuna hata mgonjwa mmoja kwenye vituo vingi vya afya walivyokuwa wametenga kwa ajili ya kuhudumia wagonjwa hao, na kusisitiza yeye mweyewe hajavaa barakoa kwa sababu hali ni shwari. Kuongezea hilo alisema kuwa kuna zaidi ya mikoa 15 ambayo haina wagonjwa wa Corona.
Tumekuwa tukiambiwa na Rais kuwa ugonjwa huu ni vita na mabeberu wamekuwa wakitufanyia hujuma bila kuambiwa hasa mabeberu ni akina nani, lakini kutokana na mkinzano huu inaonekana kabisa wale mabeberu wanaweza kuwa ni nchi ya Marekani. Kama hizi taarifa ubalozi wa Marekani unazotoa kwa kukaidi ushauri wa serikali yetu, je kuna haja gani ya kuendelea kuwabembeleza? Tumekuwa tukiaminishwa kuwa sisi ni nchi tajiri na tuna uwezo wa kusimama wenyewe bila kuyumbishwa na msimamo wa mabeberu, kwa nini serikali isiangalie upya mahusiano na taifa la Marekani? Ikumbukwe nchi ipo katika hatua za kujaribu kunusuru sekta ya utalii na matamko kama haya yanarudisha nyuma juhudi za serikali na wizara yake husika, kwa kupunguza imani kutoka kwa watalii.
Kama serikali ikiendelea kukaa kimya na kuacha ubalozi ufanye unachotaka, tunahatarisha sekta ya utalii na hata wananchi wanaweza kupata taharuki, kwa maana inawezekana taarifa hizi zinaukweli ndani yake, ni wakati muafaka ubalozi wa Marekani kuomba msamaha kwa kutoa taarifa potofu, ama serikali iutake ubalozi kufungashsa virago na kutuachia nchi yetu yenye amani na afya tele. Na kama serikali ikishindwa kukemea matamko haya basi ijitokeze hadharani na kueleza kwa nini inashindwa kukemea uovu huo unaofanywa na mabeberu, pengine taarifa zao ni za ukweli.