Nakushauri achana na hiyo dawa na ujaribu haya.
1. Chakula ndio mchawi wako namba moja. Punguza matumizi ya vyakula vya wanga na Ngano. Mfano wa vyakula vya wanga ni kama Wali. Mfano ngano ni vitu kama chapati, maandazi. Hapa nakushauri kwa asubuhi ukiweza tumia matunda ya kukatwa yale ya mchanganyiko ya buku buku. Mchana kula ugali wa dona na udaga na mboga za majani nyingi sana.
2. Kunywa lita mbili za maji kila siku. Hili fanya kuanzia ukiamka mpaka jioni. Usinywe maji usiku.
3. Tafuna karanga mbichi robo kilo kila siku huku ukisindikizia na ndizi mbivu. Hii robo igawe mara 3. Baadhi unatafuna asubuhi, jioni nyingine una malizia usiku. Huku ukiwa unasindikizia na ndizi kila utafunapo. Hii ni mbadala mzuri sana wa bisacordyl. Ukiona maendeleo yanakuwa mazuri punguzs dozi maana hii inaweza kukufanya uhalishe.
4. Fanya mazoezi ya kukimbia. Kama huwezi jitahidi utembee angalau nusu saa kila siku. Kama unafanya kazi za kukaa, huu ndii unaweza kuwa uchawi mwingine.
Naandika haya kama mtaalamu wa afya, Ukinisikiliza itakusaidia.