MamaSamia2025
JF-Expert Member
- Mar 29, 2012
- 14,588
- 32,361
Kuanzia jana nimekuwa mtu mwenye furaha sana baada ya Mama Dr Samia kumaliza biashara mapema sana kuhusu urais wa Tanzania kwenye huu mwaka wa uchaguzi. Mama kawamaliza kisiasa wapinzani wa nje na ndani ya CCM waliokuwa wanaeneza uzushi kuwa 2025 kutakuwa na mwanachama mwingine wa CCM atakayechukua fomu ya urais. Suala la urais limefungwa jana. 2025 - 2030 ni Dr Samia na Dr Nchimbi. Hakika mama ni jabali la siasa za Tanzania.
Nikirudi kwenye mada ni kuwa ninamshauri mwenyekiti wa kudumu wa chama rafiki CHADEMA ndugu Mbowe kuwa kipaumbele chake cha kwanza mara baada ya uchaguzi iwe NIDHAMU. Ahakikishe wanachama wanaheshimiana. Hali ngumu anayopitia kwa sasa ni matokeo ya yeye kufuga utovu wa nidhamu ndani ya chama. Azuie makada wa chama chake kutukana hovyo. Wajenge hoja badala ya matusi. Mwanachama wa kawaida kama Ntobi kumtukana makamu mwenyekiti taifa ni jambo ovu na la kushangaza sana.
Taasisi yenye watu wasio na nidhamu haiwezi kukua. CCM ya awamu ya Nne ilikuwa na tatizo linalofanana na la CHADEMA ila alivyoingia mwenyekiti hayati Magu hakuchekea upuuzi. Viongozi waliheshimika kuanzia ngazi ya chini hadi juu. Mama Samia naye kaendeleza suala la nidhamu. Hii imesaidia ilani kutekelezwa inavyotakiwa.