Dah nimeshtushwa sana nilipokuwa naangalia mechi za ngao ya jamii kuona nembo ya CCM pale uwanja wa Mkwakwani, Tanga. Sikuwahi kujua ule uwanja unamilikiwa na chama. Kwa hiyo maboresho yote yale ya taa na nyasi yanafanywa na nani?...
Tangu awali huu uwanja ulikuwa unamilikiwa na Manispaa na ulikuwa unaitwa Municipal Stadium kabla ya CCM kuupora.Swali zuri sana kama ni serikali ndo inakarabati kwanini usirudishwe kwa halmashauri ya jiji. Kama ni uwanja wa CCM wange ukarabati wao wenyewe CCM.
ChademaUwanja wa Mkwakwani ulikuwapo tangu enzi za Uhuru. Mwaka 1973 au 1974 ulitumika kwenye mashindano ya Taifa Cup. Cha kushangaza siku hizi unaitwa uwanja wa CCM Mkwakwakani ilihali CCM yenyewe ilizaliwa mwaka 1977.
Majuzi nimesikia kuwa serikali inaufanyia ukarabati uwanja huo; je baada ya ukarabati bao uwanja utabaki kumilikiwa na CCM au utarudishwa kwenye Halmshauri ya jiji la Tanga ambayo ndiyo lilikuwa linaumiliki kabla ya kuporwa.
Ccm wamejimilikisha kila kitu mpaka nchi ya Tz.Uwanja wa Mkwakwani ulikuwapo tangu enzi za Uhuru. Mwaka 1973 au 1974 ulitumika kwenye mashindano ya Taifa Cup. Cha kushangaza siku hizi unaitwa uwanja wa CCM Mkwakwakani ilihali CCM yenyewe ilizaliwa mwaka 1977.