GE2025 Baada ya Ummy Mwalimu kukatwa "Tutapigia Upinzani Kura si CCM"

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Samia ameshaagiza kuwa hata mkipigia kwingine kura zitakwenda CCM na cha kumfanya hamna
 
WanaCCM huwa wanadanganywa kuwa eti kuna uchaguzi. Sasa wameoneshwa kuanzia ndani ya chama chao kuwa nchi hii, chini ya CCM haijawahi kuwa na uchaguzi. Kuna wahuni wachache tu ndio huwa wanafanya maamuzi. Wengine wote wanachezeshwa tu akili. Hata mgombea wao wa Urais kateuliwa na mhuni mmoja tu, kisha wajumbe wote zaidi ya elfu 2, hawakuwa na la kusema. Na huyu akiwa Rais lazima amsikilize mhuni aliyemteua.
 
Acheni ujinga! Wenzenu wanajiandaa KUTIKI nyie mnawaza kupiga kura!
Kifupi, kura zishapigwa! Kilichobaki ni kutiki!
 
Upinzani haushiriki uchaguzi, wakipiga ACT au CHAUMMA ni kama tu wamepiga kura CCM😁
 
Genge ndani ya ccm limewafunga jela wajumbe! Haya ni maajabu! Mtu anachaguliwa na watu wake alafu wasiowake wanampiga chini!
 
Ummi akajiajiri, tena uzuri ana mtaji.
 
Huyu dada yupo poa sana alitupunguzia maumivu ya Corona alitakiwa kuwepo huko Bungeni hata kama hawamtaki sio kwa namna hiyo aisee...
 
Ummy Mwalimu kaponzwa na mdomo wake katika maandishi ya kundi sogozi la huko Tanga. Hao wapiga kura wake watulie tu, hii nchi ina miaka 64 ya uhai.
 
Huogopi kutumia jina la mtunga vitabu? Watoto wake na wajukuu wapo.
 
Una uhakika kuwa hizo kura zita "matter"?
 
Rostam azizi awezi kamwe kuruhusu uchaguzi ndani ya ccm
 
Habari leo digital:Mvutano ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilayani Tanga umefikia hatua ya wazi baada ya makundi ya wanachama kuandamana na kutangaza kurejesha kadi za uanachama wao, wakipinga hatua ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa kukata jina la aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Tanga Mjini, Ummy Mwalimu, licha ya kuongoza kwa kura nyingi katika kura za maoni za CCM za ubunge wa Jimbo hilo.

Wanachama hao, wakiongozwa na Mwenyekiti wa Tawi la CCM Chungurira, Mwinyi Zahoro Bakari, wamefika katika ofisi za CCM Wilaya ya Tanga kwa lengo la kuwasilisha malalamiko yao.

Wamesema hatua ya chama kumpitisha Kassim Amari Mbaraka, aliyepata kura 80 pekee katika kura za maoni, badala ya mshindi Ummy Mwalimu aliyejipatia kura 5,750, ni kitendo cha dharau na kupuuzia sauti za wanachama wa ngazi za chini.

"Hatuna kundi la Ummy wala la Omary, tulipeleka maamuzi yetu kwa kumpigia kura Ummy Mwalimu. Lakini huko juu wamekata jina lake. Sasa tunasema wazi, CCM isije kutulaumu Oktoba 29, 2025. Tutapigia kura upinzani kuanzia ngazi ya udiwani, ubunge na hata urais," amesema Bakari kwa msisitizo.

Wanachama hao wamesisitiza kuwa chaguo lao ni Ummy Mwalimu na wametoa rai kwa Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, kuingilia kati mzozo huo na kuhakikisha jina la Ummy linarejeshwa ili agombee ubunge kwa kipindi cha 2025-2030.

Aidha, wameweka wazi kuwa endapo chama hakitafanya marekebisho ya uamuzi huo, hawatakuwa tayari kumuunga mkono mgombea aliyeletwa na badala yake watampigia kura mpinzani.

Katika kura za maoni zilizofanyika Agosti 4, 2025, Ummy Mwalimu aliongoza kwa kura 5,750, akifuatiwa na Omary Ahmed Ayoub aliyepata kura 4,146, huku Kassim Amari Mbaraka, ambaye sasa ametangazwa kuwa mgombea rasmi, akishika nafasi ya nne kwa kura 80 pekee.

Hata hivyo, CPA Amos Makalla, aliyekuwa Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa - Itikadi, Uenezi na Mafunzo, jana alimtangaza Kassim Amari Mbaraka kuwa mgombea wa ubunge wa Jimbo la Tanga Mjini.
 
Sasa wanaenda kwa DC kufanya nini walitakiwa kwenda office ya CCM mkoa au wilaya usika
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…