EINSTEIN112
JF-Expert Member
- Oct 26, 2018
- 21,711
- 35,644
Baada ya vikosi vya jeshi la Urusi kufanikiwa kuikomboa Luhansk kutoka mikononi mwa jeshi la Ukraine; taarifa zilizopo zinaeleza kwamba vikosi vya Urusi vimeanza kuielekea Donetsk na gavana wa eneo hilo ameomba raia waondolewe haraka ili kuacha uwanja wazi kwa vikosi vya Ukraine kuweza kukabiliana navyo.
Kwa kifupi kwa asilimia kubwa mpaka sasa operesheni ya Urusi nchini Ukraine imefanikiwa kutekeleza malengo yake ya kuwakomboa wananchi wa Luhansk huku Donetsk ikiwa njiani kwenda kuachwa huru!
Kama kawaida baada ya kudonoa kidogo yale yanayojili huko Ukraine ni vyema tukarejea kuelezana mambo mengine ya msingi nje ya operesheni inayoendelea.
Bila shaka wengi wetu tulishapata kusoma habari zilizopata kutengenezwa kwenye nyakati za vita ya kiuchumi kati ya China na nchi za magharibi hususan Marekani.
Habari hizo za propaganda zilikuwa zikienezwa kila kona duniani huku zikiwa zimepewa jina tamu la 'China's Debt Trap' ikiwa ni sehemu ya mapambano ya nchi za magharibi dhidi ya China iliyokuwa ikitekeleza mpango wake uliotwa 'New Silk Road Trade Route 2013, mpango ambao ulionekana kuwa tishio kwa nchi hizo hususani kwenye yale maeneo yao ya kiushawishi Afrika nk.
Hata hivyo, mbali na propaganda hizo kupata wafuasi wengi wa kuzipigia chapuo barani Afrika na kwingineko, bado hali hiyo haikuweza kuizuia China kukubalika machoni mwa viongozi wa nchi za Afrika, Asia, Ulaya mashariki na hata Amerika kusini na kuifanya iiwashie Marekani taa ya 'kuivuka!'
Kwa mfano, mnamo mwaka 2006 nchi nambari moja kwenye biashara na Afrika ilikuwa Marekani, (2) China, (3)Ufaransa!
Lakini baada ya 'Silk Road Trade Route ya 2013;.ilipofika mwaka 2018 tayari China ikawa ni nambari moja, ikifuatiwa na India huku Marekani ikiwa nambari tatu; na hata sasa bado China imeiacha mbali nchi hiyo katika Afrika!
Wakati hasira za Marekani na nchi za magharibi zikiwa kwa China; nyuma ya pazia nako Urusi ilikuwa ikijipanga kuja kuivuruga kambi ya magharibi kwa mara nyingine! Kitendo cha kuitwaa Crimea mwaka 2014 kilifungua ukurasa mpya uliofanya macho ya wamagharibi yahamishwe kutoka China na kuigeukia Urusi!
Nchi za magharibi zilianza kuandaa jeshi kwa siri huko Ukraine kwa lengo la kuzitwaa Luhansk na Donetsk zilizokuwa zikipigania kujiondoa kutoka kwenye utawala wa Ukraine, na pengine kuja kuitwaa na Crimea pia kutoka mikononi mwa Urusi!
Katika dunia hii ogopa sana hizi nchi zenye intelijensia iliyopevuka kama Urusi nk, bimaana mchakato huo wa nchi za magharibi ulivuja na Putin akawa tayari kuhakikisha kwamba anauvuruga mapema kabla ya kuja kuleta madhara makubwa!
April 24 vikosi vya jeshi la Urusi vilivuka mipaka ya Ukraine na kuanza rasmi operesheni iliyopewa jina la 'Operation Demilitarization And Denazification!'
Hapo awali vyombo vya habari vya kimagharibi na mitandao ya kijamii ilicheza nafasi kubwa katika kuupotosha umma wa watu na kuufanya uamini kuwa Ukraine ipo vyema na ina uwezo mkubwa wa kuikabili Urusi!
Hivi sasa vyombo hivyo vimepoteza njia ya kuendelea kuwadanganya watu na zaidi vimebaki kulaumu na kuvizia matukio ya kuweza kuwafariji wasomaji wake wenye mlengo wao!
Tukiachana na propaganda za 'China's Debt Trap' zilizoishika dunia huko nyuma na ambazo hazikuziacha salama nchi za Afrika; hivi sasa kumeanza kuibuka propaganda nyingine inayoonekana kuanza kushika kasi!
Yenyewe si mpya na ni ya muda, bali baada ya Urusi kufanya mikutano na nchi za Afrika na kufunga makubaliano ya biashara; na ulinzi kwa baadhi ya nchi, propaganda hiyo imeanza kushika kasi kidogo kidogo huku ikiwa na lengo la kuzitisha nchi za Afrika kama ilivyokuwa kwenye 'China's Debt Trap!'
Propaganda inayosukumwa kwetu hivi sasa ni; 'The New Scramble For Africa' ikiwa kama ile 'Scramble For Africa' ya mwaka 1881-1914 ilivyotengenezwa kutokana na andiko lililokuwa na kichwa hicho cha habari kwenye gazeti la Times la mwaka 1884 wakati mabeberu wa nchi za magharibi walipokutana kwa uroho huko Berlin kwa lengo la kugawana ardhi ya Afrika! Propaganda hii ngaa ilishapata kuandikwa na wengi; jarida la Economist nalo limeitumia tena hivi karibuni!
Kutokana na waafrika wengi kuwa mateja wa propaganda za nchi za magharibi ni vyema sote tukajua mapema ujio wa propaganda hii mpya na kuangalia upepo utaoifanya uvume huko mbele!
Bila shaka hata maneno ya Putin kwa viongozi wa nchi za Afrika yamezichoma nchi za magharibi pale aliposema kwamba; 'hatuendi kushiriki katika kuugawa utajili wa bara lenu (kama Berlin), bali tupo tayari kujihusisha katika 'ushirikiano kwa ushirikiano' na nchi za Afrika!
Hivi sasa baada ya nchi nyingi za Afrika kuona namna Urusi ilivyozigaagaza nchi za magharibi huko mashariki ya kati hususan Syria; zimeingia makubaliano ya kiulinzi na usalama na nchi hiyo pamoja na makubaliano kwenye biashara na miradi mingineyo!
Hivyo basi, kwa wale wenzangu na mimi walio na 'uraibu' wa kuleweshwa na propaganda za kimagharibi ni vyema wajiandae kuipokea na hii pia dhidi ya Urusi!
Yajayo yanafurahisha!
Kutoka kwa mdau flani hivi mtandaoni
Hivi vita its all about uchumi sanasana na sio power
Mchina anawaburuza kwenye uchumi na wao wamemgeukia