sky soldier
JF-Expert Member
- Mar 30, 2020
- 5,407
- 19,264
Nimeanza kuvuta fegi since 2012, fegi ilikuwa daily mara 3 asubuhi, mchana, sometomes jioni na usiku, kila siku, ni mara chache mno niliruka.
Nilikuwa mvutaji wa siri sana, nilikuwa naenda kuvutia maeneo ambayo sijulikani na kweli niliweza kuitunza siri hii mpaka nimeacha hakuna anaejua kasoro wife tu aliewahi kunihisi, ila kuna nyakati tofauti tofauti unakuta ile nataka nianze kuvuta mtu naemjua anapita hio njia na tunasalimiana fresh huku nimeficha mzigo, na nikiona hivyo huo mtaa sirudii tena kuvuta, nahama kabisaa!
addiction ilikuwa sugu, nilikuwa na kigari changu, ikifika usiku naenda sehem flan napaki nafungua dirisha navuta, aisee asikuambie mtubuhitaji ndio mama wa ubunifu, kipindi cha mvua nilinununua kopo la maji makubwa nikanywa kidogo nikamwaga, nikalikata lile kopo mkono uwe unaingia pamoja na fegi ili hata mvua ikipiga isizime fegi.
kila baada ya kuvuta nilinunua pipi kali na kupiga mswaki, nilipulizia ka perfume, nilikiwa, nimetumia hela sana kununua hizi perfume na pipi.
basi mwezi wa 10 mwaka jana baada ya attempts kama 3 za nyuma kujaribu kuacha na kurudi, niliamua tu kwamba siitaki sigara, na mda huo nilikuwa navuta sababu ya mazoea tu, nilikuwa sipati kabisa ile buzz.
Mambo yalionifanya niache nilianza kufatilia sana documentaries za cancer vile naona watu wanahangaika na hadi wengine wanatolewa makoo, Pia nikawa naona nifanye sababu ya watoto wangu walau nijitunze tunze, lakini pia nilikiwa sipati kabisa vistimu hata kidogo muda huo, yani ilikuwa navuta basi tu ni mazoea.
Kwa wale mtaofananisha Bangi na sigara, jibu fupi ni kwambaunaweza kuacha bangi kirahisi na wengi wameweza lakini sigara ni ishu nyingine aisee, ile nicotine ya sigara ikiizoea mwili ni mtihani.
As of now nina miezi 7 sasa and i am so happy.