Lord denning
JF-Expert Member
- Jun 3, 2015
- 15,819
- 33,255
Watu watajiuliza kwa nini sasa TLS inakuwa maarufu sana?
Jibu ni moja tu! Umaarufu wa TLS unatokana na vyombo vya kikatiba kushindwa kusimama katika nafasi yake hivyo kupelekea TLS kama watu wanaojua umuhimu na unyeti wa katiba zaidi kuwa na sauti hivyo kupelekea wananchi kuanza kuwaona kuwa wao ndo sehemu ya muhimu zaidi katika kusimamia utawala wa Sheria.
Duniani kote. KATIBA inalindwa na Mahakama , Jeshi, pamoja na vyombo au taasisi zilizoanzishwa na Katiba yenyewe hasa Taasisi zinazosimamia msingi mkuu wa CHECKS AND BALANCE.
Kwa bahati mbaya sana. Huko nyuma, tuliwahi kuwa na mhimili imara sana wa Mahakama. Mwl. Nyerere pamoja na ubabe wake wote, chombo pekee kilichoweza kumzuia kufanya mambo ya hovyo kilikuwa Mahakama.
Hili liliendelea hadi kipindi cha Mwinyi na Mkapa!
Kwa bahati mbaya katika awamu ya 4 na 5 ndo Tanzania ilianza kuona chombo hiki pamoja na Taasisi zingine zikimezwa na Wanasiasa. Hili lilianza kuleta hofu kubwa sana kwa mustakabali wa Taifa letu hasa katika eneo la Utawala Bora.
Kitendo cha TLS kuanza kuwa vocal wakitetea misingi ya Katiba yetu hii iliyo na mapungufu bado kilianza kufanya chama hiki kuanza kuonekana kama tegemeo pekee lililobaki kwa Watanzania.
Hongereni sana TLS. Kazi iliyobaki ni kuweka nyama zaidi kwenye Katiba yetu hii ili tupate Katiba Bora zaidi itakayosimamia vizuri kwa kwa ukamilifu misingi hii ya utawala wa Sheria na utawala Bora.
Najua kwenye hili vyombo vya ulinzi vitajifunza sana kuhakikisha tunapata Katiba Bora ili kuwafunga speed governor wanasiasa!
Kuna muda Wanasiasa walijiona kuwa wamiliki wa hii nchi na huu ndo wakati wa kufanya mifumo iliyowekwa na Katiba kuwa na nguvu kuliko Wanasiasa!
Lord Denning,
Italy