Baada ya Wachina, Sasa Wavietnam Hawa Wameingia!. Watanzania Tuchangamkie Fursa!.

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined
Sep 22, 2008
Posts
53,857
Reaction score
121,995

Habari Zaidi ya Habari -Kongamano la Biasharra TZ na ...
TAARIFA KWA UMMA

Kongamano la Biashara Tanzania na Vietnam 09 Machi 2016, JNICC, Dar es Salaam

Kufuatia ziara ya Rais wa Jamhuri ya Kisoshalisti ya Vietnam, Mhe. Truong Tan Sang, nchini Tanzania, Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kwa kushirikiana na Mfuko wa Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) na Chama cha Wafanyabiashara na Viwanda cha Vietnam (VCCI), kinawaalika Wafanyabiashara wa Tanzania, katika Mkutano wa Biashara utakaofanyika katika ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere Convention Centre, JNICC, Dar es Salaam siku ya Jumatano, Machi 9, 2016, kuanzia 8.30 mchana.

Lengo la Kongamano hili ni kuwakutanisha wafanyabiashara wa Tanzania na Vietnam, kukutana, kukaa pamoja , kubadilishana uzoefu na kuanzisha mahusiano ya kibiashara na jumuiya ya biashara Vietnam. Kongamano litahutubiwa na Rais wa Jamhuri ya Kisoshalisti Vietnam, Mhe. Truong Tan Sang, na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Majaliwa K. Majaliwa (MP).

Hii ni fursa kwa wafanya biashara wa Tanzania na wale wa Vietnam kukutana ana kwa ana na kufanya mikutano ya Biashara-‐‑kwa-‐‑Biashara (B2B) katika sekta mbalimbali kama vile; Benki, Uchumi na Fedha, Mafuta na Gesi, Ujenzi na Majengo, Posta na Mawasiliano, Teknolojia ya Habari, Umeme na Electroniki, Samani, Utalii, Kilimo na Usindikaji, Chakula na vinywaji, Madawa, Nguo, viatu na biashara mbalimbali.

Ili kushiriki kongamano hili, unatakiwa kuthibitisha ushiriki wako kwa TIC kwa kuwasiliana na Brendan Maro (+255714660550; brendan.maro@tic.co.tz) au Ms.Latifah Kigoda (+255 715 734444; latiffa.kigoda@tic.co.tz) na TPSF kupitia; Mr.Onesmo Agustine (oagustine@tpsftz.org). Tarehe ya mwisho kuthibitisha ushiriki ni Jumatatu, Machi 7, 2016 saa 12:00 jioni.

Nyote Mnakaribishwa.

IDARA YA MAWASILIANO Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…