Baada ya Wakenya, ni zamu ya kujua Watanzania hutafuta nini kwenye Google

Baada ya Wakenya, ni zamu ya kujua Watanzania hutafuta nini kwenye Google

MK254

JF-Expert Member
Joined
May 11, 2013
Posts
32,408
Reaction score
50,809
Kati ya vitu vyote wanavyovitafutia maana, neno 'bae' ndio linaonekana kuwaumiza kichwa Wabongo. Halafu pia kukoroma kitandani inaonekana kama tatizo kubwa kule Tanzania.

_92997886_41eb98f1-0b76-4c0d-a590-f875193d433d.jpg
Image copyrightAFP/GETTY

Kampuni ya Google imetoa ripoti ya mambo ambayo Watanzania walitafuta sana mtandaoni mwaka 2016.
Maelezo waliyotafuta yameangazia masuala ya afya, biashara na fedha na pia burudani.

Pia, yapo masuala ya kijamii.

Walichotafuta sana mtandaoni ni matokeo ya darasa la saba 2016, zikifuatwa na Beka Boy, mtandao wa burudani.

Walitafuta pia Mkekabet, ambao ni mtandao wa kuweka dau kuhusu matokeo ya mechi za kandanda na mashindano mengine ya kimichezo.

Walitafuta pia habari kuhusu matokeo ya kidato cha nne 2016, pamoja na Raymond, ambapo walitaka habari na maelezo kumhusu mwanamuziki Hekima Raymond mzaliwa wa Moshi, Tanzania.

Walitaka kujua kufanya nini?
Watanzania walitaka sana kujua jinsi ya kuweka tone la dawa jichoni, ikifuatwa na jinsi ya kuwapata wawekezaji na wafadhili.

Walitaka pia kujua sana jinsi ya kukuza nyusi na pia jinsi ya kujua mwanamke atajifungua tarehe gani.

Huenda kukoroma likawa tatizo linalowasumbua wengi kwani, kwenye nambari tano, Watanzania walitaka kujua jinsi ya kuacha kukoroma.

Kujua maana
Katika maneno ambayo Watanzania walitafuta sana maana, nambari tatu kuna neno la kushangaza 'Bae'.

Ni ufupisho wa neno 'Babe', mtoto au mpenzi kwa Kiingereza. Pia ni akronimi ya before anyone else, kabla ya wengine wote.

Kuna wimbo wa Sauti Sol na Alikiba kwa jina Unconditionally Bae, ambao huenda uliwafanya wengi kutaka kujua maana ya 'Bae'.

Mambo yaliyotafutwa sana Tanzania 2016:
  1. matokeo ya darasa la saba 2016
  2. beka boy
  3. mkekabet
  4. salehe jembe juni 26 2016
  5. Malazi Arusha
  6. euro 2016
  7. matokeo ya kidato cha nne 2016
  8. yinga media
  9. muungwana
  10. Raymond
Walichotaka kujua sana kufanya:
  1. Jinsi ya kuweka tone la dawa jichoni
  2. Jinsi ya kupata wawekezaji/wafadhili
  3. Jinsi ya kukuza nyusi
  4. Jinsi ya kujua tarehe ya kujifungua
  5. Jinsi ya kuacha kukoroma
  6. Jinsi ya kufanya cd kuweza kuifungulia kompyuta
  7. Jinsi ya kuomba na ubani
  8. Jinsi ya kupika danish na croissant
  9. Jinsi ya kuanzisha kiwanda cha chokoleti
  10. Jinsi ya kujua iwapo mtoto amegeuka
Ni nini:
  1. Furaha kamili/upeo wa furaha ni nini
  2. Malengo ni nini
  3. Bae maana yake ni nini
  4. Elimu rasmi ni nini
  5. Ndoa ya wake wengi ni nini
  6. Hesabu ya jumla ni nini
  7. Matumizi ya pesa ni nini
  8. Soko la kubadilishana sarafu za kigeni ni nini
  9. Mfumo ni nini
  10. Ghala ni nini
Watanzania hutafuta nini mtandaoni? - BBC Swahili
 
Hahaha Mk254 umetoa wapi hii
 
Hahaha Mk254 umetoa wapi hii

Hehehe!! BBC wameianika hapo, halafu binafsi najua misamiati yote ya mitaa yote ya Dar, lakini neno 'bae' sijawahi kuliskia, inakuaje mnalitafuta kwa bidii hivi, limetokea wapi.
 
Hehehe!! BBC wameianika hapo, halafu binafsi najua misamiati yote ya mitaa yote ya Dar, lakini neno 'bae' sijawahi kuliskia, inakuaje mnalitafuta kwa bidii hivi, limetokea wapi.
Mkuu hili neno lipo. Ni kweli mwaka huu walianza kulitumia sasa wadada wakileo hasa wa hapa Kinondoni
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] maaba ya neno Bae
 
Nashukuru Porn haijawa on Top...maana jiran yangu hapa nafikiri anatafuta sana Porn kuliko chochote.
 
Basi tuko vzur hasa suala la elimu za wanetu...sio jinsi ya kutongoza ndio upuuzi gani huo..au jinsi ya kuwa mweupe...Ebo!
 
Nashukuru Porn haijawa on Top...maana jiran yangu hapa nafikiri anatafuta sana Porn kuliko chochote.
Trust me,
No1. Ni xvideos.com
No2 Ni xhamster
No3 Ni gayporn

Lakini google haitaki kuabisha watu wala kushtua wazazi wa watoto, ndo maama inaficha hizo explicit searches... Ndo maama google will never sujjest anything porn related, even if you type half the word kwa search engine, lazma u complete the word yourself Na u press the button yourself ndo inakuletea....
 
Back
Top Bottom