Baada ya Wema kummwaga Diamond, Mama Wema afanya sherehe

warumi

R I P
Joined
May 6, 2013
Posts
16,218
Reaction score
18,440
CHEREKO

Chereko! Siku chache baada ya supastaa ' grade one' wa sinema za Bongo, Wema Sepetu ' madam' kummwaga King of Bongo Fleva , Nasibu Abdul ' Diamond ' , mama mzazi wa mwigizaji huyo, Mariam Sepetu ameangusha sherehe ya nguvu kama ishara ya kuonesha ' amekunwa' na tukio hilo, linashuka nayo mstari kwa mstari.

TUJIUNGE NA CHANZO

Kwa mujibu wa chanzo makini, kutokana na mama huyo kutobariki uchumba wa mwanaye na Diamond ambaye pia anajulikana kwa jina la Dangote kwa muda mrefu , habari za uchumba huo kuvunjika zilipochapishwa kwenye Gazeti la Ijumaa ' Kubwa ' toleo lililopita, moyo wake ulijawa na furaha . "Mama Wema alichukizwa kwa kiasi kikubwa na mapenzi ya wawili hao kutokana na kile alichoamini kuwa , Diamond hakuwa na mapenzi ya dhati kwa mwanaye zaidi ya kutegemea nyota yake impe mafanikio ndiyo maana akafanya pati hiyo fupi nyumbani kwake Sinza -Mori, Dar , " kilisema chanzo hicho.

SHEREHE ILIVYOKUWA

Chanzo hicho kilizidi kumwaga unga kwamba, sherehe hiyo ilikuwa ni ya aina yake kwani mama Wema aliwaita mashosti zake, wakaandaa ' menu' ya ukweli kabisa , wakasherehekea lakini bahati mbaya Wema hakuhudhuria. "Wema hakuweza kuhudhuria sherehe hiyo kutokana na kubanwa na majukumu mengine. Bi mkubwa aliwaita marafiki zake , wakafungua shampeni, wakala , wakanywa na kucheza muziki kufurahia Dangote kupigwa chini , " kilisema chanzo hicho.

MAMA NA CHUKI YA MUDA MREFU

Chanzo hicho kilizidi kumwaga ubuyu motomoto kuwa , mama Wema alipiga cherekochereko za kutosha siku hiyo kwani alikuwa akimchukia Diamond kwa muda mrefu. "Mama Wema chuki zake kwa Diamond hazitaisha kamwe kwa kuwa hampendi tu kutokana na kuona mwanaye hasongi mbele kimaendeleo kama alivyo Diamond ambaye akiachana na Wema mambo yake hayamwendei vizuri kama anavyokuwa na mwanaye ." Diamond wakati akiwa na Jokate Mwegelo.

MAMA WEMA ANENA

Baada ya wanahabari wetu kunasa maelezo hayo ya chanzo, walimvutia waya mama Wema ambaye alikiri kufanya sherehe fupi baada ya mwanaye kummwaga Diamond . "Mimi naona huu ndiyo mwisho wa Wema na Diamond na siku zote nasema hakuna uhusiano ukadumu bila baraka za wazazi , niseme tu , sitaki kumuona ndugu yeyote wa Diamond kwangu , kama mahari wakatoe kwa Penny siyo kwa mwanangu , " alisema mama Wema .

TUJIKUMBUSHE

Kumwagana kwa Wema na Diamond safari hii ni mara ya nne. Awali walimwagana , wakarudiana , wakamwagana tena , Diamond akatua kwa Jokate Mwegelo , wakarudiana tena na Wema , wakaja mwagana tena, Diamond akatambaa na Penniel Mungilwa ' Penny' , wakamwagana, karudiana na Wema , sasa wamemwagana tena.
 
Mama nae hajitambui yani shida tupu.Baada aleee wajukuu zake kutwa yeye kwenye magazeti
 
Wacha movie iendelee, hivi season ya ngapi sasa hivi
 
Mama nae hajitambui yani shida tupu.Baada aleee wajukuu zake kutwa yeye kwenye magazeti

Kanichekesha kweli, eti ndomo mahali aipeleke kwa kina penny, dah hili tusi kubwa sana, pesa ni shetani, chezeya BMW x6 weye?? Mama wema ungetualika mimi na Dinazarde tuje kusheherekea wote maana ni shidaa au fanya uirudie party hiyo ndomo atajiju hatakiwi
 
Last edited by a moderator:
Ndomo kujishaua kote ukweni maskini unaambilia dharau na kashfa dah, kweli ng'ombe wa maskini hazai, ukaoe tu Tandale mama wema na wema hawakutaki, kwanza hujawahi kumpeleka wema china kufanya surgery ya t@ko na pesa humpi
 
Aya na zile Team mavi mavi au Team simba na Team nyani za uko insta kama alivyojisemea ray c njooni msherekee uku, mfyuu kawakomesha, si mlikuwa mnataka ndoa, mtasubiri sana maninaaaaaa,
 
Aya na zile Team mavi mavi au Team simba na Team nyani za uko insta kama alivyojisemea ray c njooni msherekee uku, mfyuu kawakomesha, si mlikuwa mnataka ndoa, mtasubiri sana maninaaaaaa,

kazi ipo na zile akaunti ig zitafungwa wau?
 

Maskini dina atalia jinsi anavyompenda domo?Kwa hiyo mm mtu anamuuza binti yake?Ila hapana chezea bmw
 
Last edited by a moderator:
Huyu Mama na mwanae wote wale wale
 

Haaaa haa binam,Boss wangu yani mie mshika pochi wako nisingekuwa nyuma nyuma kweli kama mkia!!
 
Last edited by a moderator:
Huyu mama hamjui mwanae aisee...sasa hivi atakuja aseme 'WHAT I NEED IN THIS LIFE IS ONLY MY BABY CHIBU" ngoja Ndomo acukuliwe utaona movie mpya

Utayaona tu hhhhhhhhaaaa
 

Warudie party sie tuserebukeeee weraaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
 
Last edited by a moderator:
Sasa ile harusi ya uwanja wa taifa ndo basi tena tunaukosa mnuso??????? Ila ubuyu huu mtamu kama wa ZNZ
 
Huyu Mama sijui kama anajua kama anajidhalilisha wenzie wanauza sura yeye anajitia BP,kwanza amuulize mwanawe kilimrudisha nini kwa Huyo Diamond mara 4,mtu mzima lakini hatumii busara kabisa ..............
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…