Baada ya wosia wa Lady Jaydee: kauli ya Gardner G. Habash

Twilumba

JF-Expert Member
Joined
Dec 5, 2010
Posts
12,576
Reaction score
14,522
Katika pita pita leo nikakutana na kauli ya Gadna G. Habashi meneja lkn pia mume wa mwamamuziki Jide aliyetoa wosia siku za karibuni kuhusiana na mtafaruku ulioko kati yake na Clouds Media,na hayo ndiyo niliyoyachota;

Kupitia kipindi cha The Takeover kinachorushwa na kituo cha TBC fm haya ndio yalikuwa majibu ya maswali niliyomuuliza GadNa G; Ipi ni Kauli yako juu ya Wosia wa Lady Jay Dee...?

Gadna G: Ni maneno ambayo yametoka moyoni mwake na ni maneno mbayo anajitetea kama msanii, mimi kama Meneja ukiacha pia kama mke wangu naendelea kumsapot kwa kile ambacho anaona ni sawa, basi mimi nitaendelea kumsaport na kujaribu kuzungumza na Lady Jay Dee, mara nyingi anasema tu kwamba watu wasifikilie ni swala la wimbo kupigwa au kutokupigwa, hayo ni mambo ya kawaida lakini wafikirie tu kwamba huyu mtu anaongea kutokana experience yake aliyokuwa nayo na wale watu.

Baada ya mwaka 2003 kuacha kufanya kazi kwenye management yao ya Smooth Vibe, yalitokea mambo mengi hapa katikati ila hakusema lakini siku za hivi siku za karibuni kuna mengine ambayo yametokea, ndio akaona hapana nisipo sema nitazidi kukandamizwa na matokeo yake nitakufa kisabuni.


Hii ni kama vita mmejipangaje..?

Gadna G: Unapoamua kusema ukweli swala la kujipanga mara mbili huwa halipo, ni kwamba unasema ukweli watu wasikie naukizungumzia uhasama watu watauliza juu ya uhasama lakini ulikuwepo tayari kwahiyo tu watu wanajua kwa sasa kwa kuwa jdee ameamuwa kuongea lakini tu hawajui tu kwamba jdee alikuwa na matatizo na wale watu tangu kipindi cha nyuma sababu wale watu wanafumo dume ya kufanya kazi na alipoachananao aliona kama wanamfatilia kulekule ambapo yeye alipo

Nini mlikiona kama chokochoko...?

Gadna G: Unajua kwa mfano unaweza kumuomba mtu maji akakwambia sina, ukayaona yale pale ukamwambia niuzie akakuuzia ila bado alivyokuuzia akaona kama unafaidi, mwisho akakwambia yameisha nenda sehemu nyingine, ukaenda sehemu nyingine na ukayapata bure, akaona umepata akaamua kukufata kulekule na akakukuta unakunywa maji kwenye grasi kisha akakuputa, sasa hapo inabidi useme hapa unavyofanya sio sawa ndo hicho anachofanya Jay Dee sasa hivi.

Hali hii imewaathiri kwa kiasi gani...?

Gadna G: Cha kushukuru Mungu ni kwamba msanii au hata pia stesheni ya redio inategamea umma wa Watanzania au hata mashabiki kwa ujumla kwa kuwepo kwake.

Jay Dee anapata saport nzuri kutoka Watanzania, basi ujue hata hajaathirika chochote, na pia tu anaendelea kufanya kazi kwa bidii, ila tu isipokuwa unapoona mtu anafanya madhara ili tu mtu apate athari fulani ndio unasimama kuongea, ndiyo maana tuna Bunge na watu wanasimama, watu wanaongea, watu wanatetea hoja, ndiyo maana yake. Yani lazima mtu usimame useme ukweli kwa unalohisi hili jambo litanipa madhara nisiposema.


Kwa Wasanii wengine unawaambiaje...?
Gadna G: Uwoga ni kitu ambacho binadamu tumeumbiwa, wakati mwingine unasaidia wakati mwingine unakudhiru uwoga wako,kwa sababu wanasema adui wa maendeleo yako mwenyewe ni wewe mwenyewe, ndiyo maana uwoga wako unaeza ukasabishwa ukakandamizwa zaidi, ndiyo maana wazee wetu waliweza kusimama na kuikomboa hii nchi kwa sababu walisimama hawakuogopa.
Wangeogopa hii leo hii nchi tusingekuwa huru, kwa hiyo kama kuna mtu ana jambo na anaogopa kusema hilo ni jambo la kawaida kuogopa, lakini wakati wa kusema ukifika usiogope kusema ili mradi useme ukweli, basi inatosha....
Kauli yako ya mwisho ni ipi..?

Gadna G: Ni kwamba wanahitaji kujua ukweli na kuambiwa ukweli, mtu yoyote anayejua kitu cha kweli anaweza kusema sio sawa, utaendelea kukandamizwa. Kauli ya mwisho ndo hiyo wanahitaji kuambiwa ukweli na kusikia ukweli ili kama wanakosea wasiendelee kukosea wabadilikee….

Mwisho ...
SOURCE: PamojaPure Blog
 
safi sana gadna usichoke
 
Ukweli siku zote hukuweka huru, japo huwa ni mchungu kwa wengine.

sema jamaa wanahagaika na kukanusha indirect wenye media yao lkn to late wabongo wanajua mbivu na mbhichi hv sasa!
 
Gardner ameongea vizuri sana.
Clouds fm wameumbuka sasa.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Ukweli utajitenga tu na uongo

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Binti Komando dont give up katu usije wapigia magoti kenge wa mjini.
Ur strong emotionally and spiruatually.
Kikubwa zaidi una kipaji na u mbunifu .
tunakujua tunakuheshimu na kukuthamini.
Daima tuko pamoja kwenye hills and valleys
 
Kuna mshikaji wangu mmoja mtu wa media nilikuwa nae jioni hii nae pia amenijuza kuwa moja ya baya ambalo Ruge alimfanyia Jide ni baada ya kumshawishi mmoja wa wafanyakazi wa Zantel (Mwenye nafasi ya juu) kuwa ahakikishe zantel hawai-renew mkataba wa kufanya nae Adverts especiall billboard.

Ambapo jamaa huyo wa zantel bila kujua athari zake alikubali na mara ya kuisha tu ule mkataba Zantel kweli walisitisha mkataba na Jide, lakini Jide alikuja kuzinasa kuwa mbaya aliyeharibu utaratibu wa Ku-renew mkataba wake ni Ruge!

MY TAKE:
Kwa namna hiyo Jamaa kiukweli kama alifanya hivyo ana roho ya kwa nini na haina budi aelezwe ukweli, kama ni wa kujirekebisha basi ifike sehemu ajirekebishe!!
 
Mbona kuna tangazo la Gadna linasikika clouds fm, kuwahamasisha watu waende kwenye burudani? Au ile sio sauti yake?
 

......wabongo tujifunze kuwa wawazi na wakweli.....hii mambo ya nasikia nasikia.....haisaidii.....Mbona Mh Sugu alitoka kiwazi wazi kabisa na watu tukaelewa mbivu na mbichi.......lakini hii mambo ya kuchimbana mkwara...mara usije kwenye msiba wangu ni.....upuuzi......

watu wanatakiwa wauze "product" na sio "uzuri" au "jina"
 


namchukia Ruge kwa maovu yake ambayo nilipata kumsikia Sugu akiyasema hadharani bila kumung'unya.

Lakini mkuu siwezi zidisha chuki zangu kwa habari kama hii ambayo haijathibitishwa.
JUDITH alipaswa kuweka wazi kila baya alilofanyiwa na Ruge na Kusaga.

Jamani hebu tutofautishe kati ya tuhuma na shitaka...
 

Ndo wale wale
 

Exactly!......Heshima Mbele Mkuu.......

watu wamebaki kulaani wengine kwa hadithi za "nasikia.....blah blah blah....... nasikia blah blah blah.....hisaidii kitu
 


Kuna mtu anaitwa MTAZAMO...
Akija hapa atasema ''Gang Chomba = Ogah''
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…