Nadhani wapo wengi wenye vipaji, Kina Marlow, Z Anto, Mike T, Stara Thomas na wengine....Ni nini ushauri wenu kwao ili tuendelee kuwaona ?Tusing'ang'anie tu wasanii wananyonywa...Nini mipango na ushauri wenu kuwasaidia ?Au mkishashabikia Ruge ni mnyonyaji inatosha ? Nguvu inayotumika kumshutumu Ruge na clouds ndio msaada kwa hao wasanii ? Watanzania tumejaliwa vichwa vilivyokosa ufumbuzi wa matatizo.Kazi kubwa ni kutafuta visingizio na sababu. Hayo maslahi ya wasanii (ambayo zaidi ni hisia) yatakuwepo kwa kumuondoa Ruge na clouds ? Ushauri wangu kwenu...badala ya kuonyesha chuki zenu zisizo na mashiko, Ni bora mngeonyesha kuguswa kweli kweli na hayo matatizo ya wasanii kwa kuanzisha umoja ambao mtachangishana au kutafuta mkopo na kufungua STUDIO au RADIO ambayo itakuwa na mfumo mzuri wa kuhakikisha wasanii wananeemeka. Kukaa pembeni na kujifanya mnawasaidia wasanii kulia ni unafiki tuu. Unafiki huu mimi naufananisha na kero ya muda mrefu ninayokutana nayo kwenye daladala, Konda anapomzuia mwanafunzi utasikia abiria wote kwenye basi wakimshutumu konda, huna huruma, huna watoto, ndio maana hukusoma na maneno kadha wa kadha...Huu ni unafiki mkubwa uliotujaa watanzania..Wewe abiria unayeenda kazini...unalipwa mshahara mzuri (kwa maana zaidi ya anavyopata konda) Kwa nini usimlipie yule mwanafunzi ili apate heshima unayopata wewe kutoka kwa konda ? Nani asiyejua ugomvi wa konda na mwanafunzi ni nauli ? Unamuhukumu vipi konda anayekwambia kwamba malipo yake yanatokana na alichokusanya....Mbona wewe ni mkali kweli kweli huko kazini au kwenye biashara yako unapopunjwa pesa ? kama kweli unaguswa na manyanyaso anayopata mwanafunzi ingia mfukoni uone kama konda atamsumbua tena. kupiga tu kelele kwa kumkemea konda ni UNAFIKI tu wa kujionyesha unamjali wakati sio kweli. Sisemi ni sawa kwa konda kumsumbua mwanafunzi, Bali ninachohoji hapa ni nini ufumbuzi wako pale unapokuwa kwenye daladala na ukaona mwanafunzi anazuiliwa kuingia ?Binti Komando dont give up katu usije wapigia magoti kenge wa mjini.
Ur strong emotionally and spiruatually.
Kikubwa zaidi una kipaji na u mbunifu .
tunakujua tunakuheshimu na kukuthamini.
Daima tuko pamoja kwenye hills and valleys