Baada ya zama za kubebwa na Yamoto Band kupita, Enock Bella atoa wimbo mbaya kupitiliza

Hance Mtanashati

JF-Expert Member
Joined
Sep 7, 2016
Posts
20,137
Reaction score
26,189
Ama kweli majumba makubwa hustiri mambo hii kauli kwa namna fulani inashibahiana na hali inayomkuta sasa msanii Enock Bella

Huyu kijana kipindi yupo yamoto band aliwahi kutamba sana na sauti yake nzito na tungo tata zilizowachanganya vilivyo akina dada.

Mwanzoni huyu kijana alikuwa ni dancer tu wakawaida ila mkubwa fella akatumia kila aina ya ushawishi ili huyu jamaa naye aimbe kama wenzake kwenye kundi na akamsifia vilivyo kwamba sauti yake itaziba pengo la marehemu Muhiddin Gurumo lakini siku zote bwana mtu kama huna kipaji huna tu hata ufanye nini.

Alipokuwa Yamoto alijificha nyuma ya wenzake na kuimba maneno mawili matatu na hakuweza kugundulika kirahisi kwamba jamaa ni debe tupu ila tangu kundi livunjike huyu jamaa ana hali mbaya sana kimuziki na hilo limejidhihirisha mara baada ya kutoa wimbo kama solo artist uitwao Sauda.

Aisee huu wimbo ni mbaya mbaya mbayaa kupita maelezo hausikiliziki hauchezeki kwa kifupi hauvutii kabisa au kwa maneno mengine naweza kusema huu ndio wimbo mbovu zaidi kwa mwaka huu 2017/2018.

Jamaa bora aangalie tu ustaarabu mwengine mziki hawezi.

Huko IG watu wachache wamejitokeza kumsapoti lakini wapi ngoma haisapotiki ,imedoda.
Pole sana Enock Bela tafuta kazi nyingine tu huku kwenye mziki unatukera huna ulichobakiza.

 
Ngoja nikachunguze hayo maneno yako kwanza
 
Umekosea sanaa.. Jamaa ndoto yake kubwa kua mwanamusic kama akina diamond na kiba.... Hvyo ni kumpa ujanja nini afanye ili atoke.... Ama awe dancer... Ama abadili Style ya sauti yake.... Ama atumie computer kuweka sauti sawa
 
Nashukuru kwa kunifahamisha kuwa katoa wimbo ngoja nikausikilize
 
Hiyo mbona kawaida tu kuwa hivyo. Wala sio laana au mkosi.

Dogo nilipenda sana vipande vyake kwy yamoto ila kwa huu wimbo wake kweli ni mbaya hata mie nimeusikiliza leo. Namuombea tu apate namna na yeye atokelezee ..

Ila wasanii wa aina yake wapo wengi tu hata huko ugaibuni

Hapa nyumbani kuna kama yule anayejiita "mh T", Taasisi M, yule dogo wa kwy Ohoo...oooho nzelaaaaa...
Tafuta single zao uchoke!

Na wengine ni yule "supa nyam..." marehemu Ndanda K (sijui kama una kumbukumbu ya wimbo wake wowote kichwani alioimba baada ya kuanzisha bendi yake kwa mbwembwe - mie nilifikiri anafanya matangazo ya mavazi kupitia nyimbo).

Kuna yule mwingine aliyekua anaitikia kwy wimbo wa jela kubaya "tulifungwa jelaaaa...." sikiliza single zake baada ya kujitenga kama utajaribu hata kuokota zikitupwa.
 
Ukitaka kuponda kitu, ni bora uponde kwa kituo, kwa detail,kwa facts.

Ama sivyo utaonekana hater tu.

Weka wimbo hapa halafu elezea kwa kina kwa nini wimbo ni mbaya, anzia ala, upangiliaji, uimbaji, vionjo etc.

Siyo unaponda jumla tu kama muuza magunia soko la Kariakoo.

Nitakuponda kwamba hujui kuponda.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…