Baada ya ziara mikoani, viongozi mrudi ofisini kweli na kuchukua hatua

Baada ya ziara mikoani, viongozi mrudi ofisini kweli na kuchukua hatua

Joined
Jul 6, 2024
Posts
97
Reaction score
72
VIONGOZI CCM TAIFA MNAFANYA VIZURI SAANA KUTEMBELEA MIKOANI NA KUYASOMA MABANGOBAADA YA HAPOTURUDI OFISINI TUWE NA TAFAKURI NZITOKISHA TUCHUKUWE HATUA ZA KUFANYA MAAMUZI MAGUMU

Nilisikika nikiunguruma Kama Simba Katika Ulimwengu wa kiroho huko Ndotoni kukemea Maovu ya kuzisigina katiba Kanuni miongozo na Taratibu kwa kulindwa Maovu ya Baadhi ya Viongozi wenye fedha.

Nikaanza Nakumbuka Tarehe 04/05/2024Comrade Abdulrahman Omar KinanaMakamu Mwenyekiti CCM Taifa Bara Alisema Sheria ipo lakini sheria lazima iende na utashi na ridhaa na Uungwana ndani yake .Unaweza ukawa na sheria (lakini) ukaipuuza. Mwisho wa kunukuu.

Comrade Paul Christian Makonda Akiwa Rukwa Nakumbuka Tarehe 05/02/2024Alisema Kama tukifanya (kazi zetu) Kama tulivyoapa. Kama tukitenda kazi Kama misingi ya Katiba yetu (ya CCM), Mimi nawahakikishieni ile (kusema) Binadamu (wote) sawa itaonekana mpaka Mtaani. Mwisho wa kunukuu.

Nakumbuka Tarehe 05/02/2024Comrade Paul Christian Makonda Alisema Adui wa Chama Cha Mapinduzi sio Chama Cha Upinzani. Adui wa Chama Cha Mapinduzi ni Watendaji wazembe na Wavivu wasiotimiza wajibu wao Katika Madaraka waliyopewa. Chama hiki hakiwezi kutoka Madarakani kama Watendaji wote wa Serikali watafanya (kazi zao) kwa mujibu wa sheria na Taratibu na kutanguliza utu (na) sio tumbo lao.

(Watumishi) wakitanguliza utu Wakaweka kipaumbele Cha kumtazama Binaadamu bila kujali kipato chakeBila kujali Elimu yakeBila kujali kabila lakeWakasema Binadamu wote ni sawa,Chama hiki (Cha CCM) kitaendelea kutawala Milele na Milele. Kwa sababu wananchi wana Shida ya huduma zao (na Wala )sio rangi ya chama Wala sura ya mtu Katika madaraka.Mwisho wa kunukuu.

Tukisoma Kitabu cha Tujisahihishe uk 13 Mwl Julius Kambarage Nyerere Aliwahi kuandika Chama ambacho Nia yake ni kuwa Daktari wa Matatizo ya Jumuiya hakina budi kujuwa sababu ya Matatizo yenyewe na Dawa yakeBila kujuwa kujuwa Matatizo na sababu ya Matatizo hakiwezi kujuwa Dawa yake. Mwisho wa kunukuu.

Sisi Kama chama tunao wajibu wa kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi Sehemu iliyo sahihi.Chama chetu kina Viongozi Tokea Shina, Tawi, Kata, Jimbo na Wilaya nk. Tusome ilani ya CCM 2020 uk 303 ibara 255, uk 298-299 ibara 251(e) uk 04-05 ibara 07 ili kupata ruksa ya kwenda kusoma ilani ya CCM 2015 uk 296 ibara 189 uk 233-234 ibara 185(b) uk 230 ibara 177 Kisha turudi ilani ya CCM 2020 uk 01 ibara 04 na uk 161-168 bila kuacha uk 08 ibara 10 na 11 kwa msisitizo kwa mazingatio ya uk 298 ibara 251 ikisomwa kwa Pamoja na ilani ya CCM 2015 uk (i) ibara 01.Enzi za waasisi wetuWananchi waliona fahari kwenda Ofisi za CCM kupeleka kero zao.

Tuiridishe Imani hii kwa kuelekeza fikra zetu katikakuboresha Ofisi za Tawi , kata , Jimbo na WilayaUsaliti Mkubwa kwa CCM ni Kiongozi kuwa na Cheo chenye Uwezo wa kuwainua Wanaccm Mafukara ila kwa Ubinafsi wake akaanza kuwatumia Wanaccm Mafukara Kama Vibaraka Vikaragosi na Vijibwa vya kumfanya Yeye azidi kudumu kwenye Cheo huku Akiwa na Nia ovu ,akijifanya anawasaidia wanajamii wengine huku akiwanyari Wanaccm Mafukara wafia chama Tusome kanuni za Uchaguzi wa CCM toleo la December 2022 uk wote wa viii - ixTuboreshe Motisha za Watumishi wa CCM tokea Shina mpaka Wilaya.

Mfano Mwanaccm Katibu Tawi analipwa Tshs 5000 kwa Mwezi Tena sio kwa wakati Viongozi waliobaki wote hawalipwi🤔🤔🤔Katibu kata analipwa Tshs 10,000 kwa Mwezi waliobaki wengine hawalipwi🤔🤔🤔Mwenyekiti CCM Wilaya analipwa Tshs 50,000 nkHaya ndiyo Mazingira ambayo hupelekea baadhi ya Wanaccm kuto kutenda haki na kuishia kuwa Wala Rushwa.Na kuto kushinda Maofisini kusikiliza kero.Nakumbuka Tarehe 01/02/2024.

Mheshimiwa Rais Ambaye ndiye Mwenyekiti CCM TaifaDkt Samia Suluhu HassanSiku ya Maadhimisho ya SheriaAlisemaNi vizuri kubuni mbinu za kutoa motisha kwa Watumishi Hawa na wengine wanaofanya kazi zao kwa ubunifu Uadilifu, na Ueledi wanao wezesha Taasisi kuongeza UfanisiSasa (watu wabunifu , waadilifu na weledi ) msipowatunza ( mjuwe watu)wengine wanao watolea macho watakuja kuwachukuwa na kuwapa madonge manono na nyie muanze upyaNa mkianza upya mtarudi pale mlipofikiaMtarudi nyuma.Mwisho wa kunukuuComrade Dkt Bashiru Ally KakurwaAkiwa Katibu Mkuu CCM Taifa aliwahi kusema kauli ya Rais ni kauli ya CCM.

Kwa Msingi huu CCM inajua umuhimu wa posho na uwezeshwaji kwa watu wenye umuhimu na Taasisi.Wanaccm Mafukara hujitoa kwa Umahiri Mkubwa kuisaka Dola na wanajuwa baada ya kushika Dola wao huachwa solemba wakiwa na njaa.Wenyeviti wa Serikali za Mitaa BaadhiMadiwani BaadhiNa Wabunge BaadhiWasiokuwa wazalendoBaada ya kuyaona hayaWakatumia fursaWakaingilia Chaguzi za sssem.

Wakatoa Rushwa kuweka Viongozi ndani ya ssseemWasiojuwa vyeo vyao hata wakiulizwaWasiojuwa ilani , katiba ya CCM, Kanuni miongozo na Taratibu Wenye kuwaza Ubwabwa Walamba visigino Wasiotetea lolote ndani ya JamiiNa Viongozi hao walio wengi huishi kinyume na Matakwa ya ibara 07 na 08 ya katiba ya CCM 1977 toleo 2022 lakini ndiyo Viongozi wanaotegemewa waje wakae kwenye vikao kututafutia Viongozi waadilifu na Waaminifu watakao wainua Mafukara kiuchumi.

Huku ndiko kupanga safu kuliko pelekea Wanaccm na wananchi kukata Tamaa kupeleka kero zao Ofisi za ssseem.Nini kifanyike SasaViongozi wa KitaifaShukeni ngazi za Matawi na kataItisheni mikutanoKuweni wapoleSikilizeni Wanaccm Mafukara Vilio vyaoWatoeni wasiotakiwa kwenye nyadhifa .KishaWekeni Viongozi wanao kubalika na Wanassem walio wengi.

Tokea hapo SasaViongozi wa Kitaifa muwe mnasikiza Vilio vya Wanassem na wananchi na Kisha kuchukuwa hatua.Viongozi Hawa ngazi za Chini ndiyo wawe na Majukumu ya kukagua Utekelezaji wa ilani kwenye maeneo Yao baada ya kuwawezesha kiuchumi.

Kiongozi Mzembe hatakuwa na nafasi TenaIla tukiendelea kulindanaWatu wanauza Ofisi za ssseem tunanyamaza Wanauza typewriter za CCM tunanyamaza Wanawaonea Wanaccm Mafukara tunanyamaza Halafu tunajionyesha kusaidia watu Baki huku sisi kwa Sisi tukiwa hatusaidianiWala kusikilizanaHuku ndiko kuendesha chama kisanii.

Naomba Viongozi wa Kitaifa niiteni niwaonye fedha zilipo za kuboresha chama na kuongeza Pato ili Viongozi walipwe bila kubaguliwa tokea Shina , Tawi, kata, JimboTusome katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ibara 18(a) na 19(1) kwa mazingatio ya ibara 09 a b f na hKatiba ya CCM ibara 5(8)Ilani ya CCM ibara 110(c)Comrade Paul Christian MakondaKatibu NEC Itikadi Siasa na Uenezi CCM TaifaNakumbuka Tarehe 05/02/2024AlisemaChama (Cha CCM) kikiacha kushughulika na kero za wananchiChama kikiacha kuhangaika kutafuta Majibu ya Changamoto za wananchiChama hicho kinapoteza uhalali wa kutawala. Mwisho wa kunukuuKero za watu ni Pamoja na kero zetu ndani ya CCM.

Tuziondoe kero za safu ambazo huwekwa na watu wenye fedha za Rushwa na kuishia kuwaonea Mafukara wasio na Mtetezi. Nikashtuka Ndotoni nikiwa nimelowa Jasho nikiwa kimyaaa.

Kidumu chama Cha Mapinduzi

Mathias Mugerwa Kahinga
🙏🏿🙏🏿🔨🔨💪🏿💪🏿
 
Back
Top Bottom