Elections 2010 Baadhi mawaziri na wabunge waliopita wanaona ufa mkubwa ktk serikali inayomaliza muda

Elections 2010 Baadhi mawaziri na wabunge waliopita wanaona ufa mkubwa ktk serikali inayomaliza muda

Mtaka Haki

JF-Expert Member
Joined
Oct 1, 2010
Posts
492
Reaction score
149
Tulikuwa kwenye ndege ya Precission nikiwa na rafiki yangu. Tukawa tumekaa jirani na waziri mmoja mwadilifu wa serikali ya JK. Tukaamua kuanzisha mazungumzo ya ufisadi na kumweleza waziri kwa ukweli jinsi tulivyokatishwa tamaa. Tukamweleza kuwa ukweli namna serikali yenu ilivyoshughulikia Ufisadi basi mwaka huu sidhani kama tutaweza kwenda kinyume na dhamira zetu na kuwapeni kura.
Yule waziri alisogea karibu na masikio yetu na kusema. Ukweli hata sisi wengine tunasikitishwa mno na aina ya uongozi wetu usivyokuwa serious.
Akalalamikia masuala ya ushirikina kupewa kipaumbele sana katika uongozi na hata kuzingatiwa ushauri wa kishirikina kuliko wa kitaalamu, hatimaye akasema hata sisi tunambeba tu sio kwamba tunaona kama ana uwezo huo. Ila kwenye siasa lazima tufanye hivyo la sivyo tutapoteza chakula cha watoto wetu.
SUALA LA UKABILA NA UDINI LINALOENDELEZWA NI MBINU CHAFU YA KUONYESHA NI KWA NINI MTU ANASHINDWA. VISINGIZIO VINATENGENEZWA KUWA NI IONGOZI WA DINI WANATAKA KUUANGUSHA UTAWALA ULIOKO
Mbinu hizi chafu za udini na ukabila hata hapa kwenye thread zinatumika. HUKU NI KUFILISIKA KWA HALI YA JUU.
MTU HAUKUMIWI KWA DINI YAKE AU KABILA LAKE BALI KWA UWEZO WAKE.

MAKAMBA ALIPOKUWA MOSHI ALIWAONYA VIONGOZI WA DINI. SABABU KUBWA YA VIONGOZI WA DINI KUONEKANA KUWA KINYUME MWAKA HUU NI KULE KUWA WAZI " CALLING A SPOON "SPOON" AND A SPADE " SPADE"
VIONGOZI WA DINI WAMEENDELEA KUSEMA HATUUNGI MKONO VYAMA TUNAUNGA MKONO MTU.
HUU NI MWAKA AMBAO VYAMA DINI, MAKABILA HAYANA NAFASI. NI MTU MWENYE UWEZO.
Ninasikitika mawaziri hao na wabunge ambao wameshindwa kuwa kama Mpenda Zoe.
NAOMBA WATU WALIO KARIBU NA JK WAMTIE MOYO KUWA ITS OK KUSHINDWA. DONT TAKE IT PERSONAL.
 
Matatizo haya yalianza wakati wa Utawala wa Mzee Mwinyi -- yeye aliendeleza UDINI sana... Alimlea na kumkuza Kikwete kuwa Rais na Kikwete kafuata Masuala na Maamuzi ya Mzee Mwinyi... haya Nchi yetu sasa imevurugika sijua kwanini tunapenda Muungano na Zanzibar; Angalia tulivyo na dini nyingi tunaweza tukawa ovyo kulikoni Rwanda na Burundi...
Sasa ndio nakumbuka kwanini Nyerere hakukimbilia hayo Madini alitaka kwanza tujenge AMANI tuelewana wakati MASIKINI tutaweza kuwa na UMOJA... walafi wamechukua nchi kidogo kidogo tunanyofoana angalia Tarime... kuna Mgodi watu wa Tarime hawanufaiki hata walinzi ni watu wa Kenya...

"All of us who are concerned for peace and triumph of reason and justice must be keenly aware how small an influence reason and honest good will exert upon events in the political field"
 
Yule waziri alisogea karibu na masikio yetu na kusema. Ukweli hata sisi wengine tunasikitishwa mno na aina ya uongozi wetu usivyokuwa serious.
Akalalamikia masuala ya ushirikina kupewa kipaumbele sana katika uongozi na hata kuzingatiwa ushauri wa kishirikina kuliko wa kitaalamu, hatimaye akasema hata sisi tunambeba tu sio kwamba tunaona kama ana uwezo huo. Ila kwenye siasa lazima tufanye hivyo la sivyo tutapoteza chakula cha watoto wetu.
SUALA LA UKABILA NA UDINI LINALOENDELEZWA NI MBINU CHAFU YA KUONYESHA NI KWA NINI MTU ANASHINDWA. VISINGIZIO VINATENGENEZWA KUWA NI IONGOZI WA DINI WANATAKA KUUANGUSHA UTAWALA ULIOKO
Mbinu hizi chafu za udini na ukabila hata hapa kwenye thread zinatumika. HUKU NI KUFILISIKA KWA HALI YA JUU.
MTU HAUKUMIWI KWA DINI YAKE AU KABILA LAKE BALI KWA UWEZO WAKE.

I liked this part, man!!!!
 
Back
Top Bottom