MK254
JF-Expert Member
- May 11, 2013
- 32,408
- 50,809
Nimeona baadhi ya Wakenya wa Mombasa wakitishia kugoma kupimwa Corona na kutolea mifano ya Tanzania ambako matikiti maji, mapaipai n.k. zinapmwa na kukutwa na Corona.
Ndugu zangu Wakenya, muhimu tuchangamkie hili zoezi la "mass testing" ambalo linaendelea, tupange foleni na kupimwa kila mmoja wetu, binafsi nakusudia kupima Jumapili ijayo, acheni kuingia kwenye siasa za Tanzania kichwa kichwa, ifahamike wale wamesalia na miezi michache kabla kuingia kwenye uchaguzi mkuu, hivyo kila kitu kwao kwa sasa kinapelekeshwa kwa milengo, mitazamo na misimamo ya kisiasa, hata janga kama hili ambalo ni hatari kwa dunia, ukipitia majukwaa yao ya kisiasa na mitandao ya kijamii, wanajadili hiki kirusi kwa mihemko ya kisiasa.
Tikitaka zao za mananasi, mapaipai oili ya gari n.k. visisababishe tususie hii shughuli kwetu, muhimu tukafahamu juzi tumeona CDC wametolea takwimu za Tanzania kwamba huko hadi sasa wamepima watu 652 pekee yake na kupata idadi ya walioambukizwa kuwa 480, hiyo inaonyesha uwezekano wa kwanini mkulu wao ana hasira, angalia hotuba zake zimejaa hasira balaa.
Ukipitia majukwaa yao ya kisiasa humu JF, nyuzi za tanzia huibuka kila siku, mara waziri kadondoka na kufariki, mara mbunge, pia tunona wanavyotupia video na mapicha ya mambo yanayotendeka kwao, ukikumbuka RC wa Dar mwenyewe aliwahi kunukuliwa akitahadharisha watu wa mikoani wasije Dar maana huko wanapukutika kama majani, ni mwendo wa mazishi.
Jameni jameni chonde chonde Wakenya muhimu tukafahamu kwamba kwa kupimwa na kujua hali yako, itakusaidia kuwalinda uwapendao, inawezekana wewe ukawa na uwezo mkubwa wa kupambana na kirusi, lakini pia ukawaambukiza familia yako na kuwazika kadhaa, ujikute unamzika mkeo au mumeo, au mwanao, hivyo kuna umuhimu mkubwa wa kujua hali yako kama ilivyo kwa UKIMWI, pima pima pima, hata ikiwezekana kila wiki pima mara moja maana sasa vipimo vimeshaingia mtaani, ushindwe wewe tu.
Pia natoa wito kwa serikali, itie jitihada za kuhakikisha inagharamikia siku ambazo Wakenya wanaishi kwenye karantini, kama vipi mteue shule kadhaa za bweni na kuzigeuza vituo vya karantini, kisha turuhusiwe kuwaletea wapendwa wetu vyakula ili kupunguzia gharama, mjiongeze kimikakati ili Wakenya wachangamkie hili zoezi.
Halafu mheshimiwa Joho gavan wa gatuzi 001, natoa rai achana kabisa na mikwara kwa watu wako wa Mombasa, hasira hazitosaidia kitu, waelimishe taratibu, kama kunao wapambe wa huyu gavana humu, jaribuni kumshauri hili zoezi halitafaulu kwa kutumia hisia kali, Wakennya sio kama Wabongo ambao kule kwao wakikaripiwa na mkulu wanaufyata wote mpaka hata Corona yenyewe inaingia mitini, kwa Wakenya ukiwajia kwa hasira ndio utakua unawapandisha full mzuka na utashindwa kuwatawala au kuwaelekeza.
Naona Watanzania wameanzisha nyuzi za kujiliwaza kuhusu hili
Magufuli aistua Dunia kuhusu vipimo fake vya Corona!, Mombasa wagomea kupima Corona, wamtaja Magufuli amesaidia kustuka, wathibisha JPM is Right!. - JamiiForums