A
Anonymous
Guest
Hii tabia ya Askari wa Barabarani especially Mkoa wa Dar es Salaam maeneo mengi likiwemo eneo la Kamata Kariakoo, Ilala Boma na maeneo mengineyo, kutafuta vijana machawa wa kukamata Bodaboda ambao wamevunja Sheria za Usalama Barabarani kama kutokuvaa kofia ngumu na mengineyo, sio nzuri na ipo siku itasababisha madhara makubwa.
Unakuta askari amekaa kwenye kibanda kawaacha watu ambao hawana mafunzo yoyote ya Jeshi la Polisi kazi ya kukamata Bodaboda, hii inasababisha sana rushwa maana mwisho wa siku wale vijana lazima walipwe au wajilipe.
Je, hela wanatoa wapi kama si kuchukua rushwa! Lingine ni kuchochea chuki kwenye jamii baina ya wakamataji na Bodaboda.
Jeshi la Polisi hili lifanyiwe kazi, kama Viongozi wa Juu ndani ya Jeshi la Polisi hamjui hili basi chukueni hatua haraka, kama mnajua basi tambueni mnachokitengeneza ipo siku kitakuwa mwiba mchungu kwenu.
Yanaweza kutokea madhara na yakawa na athari kubwa.