cView attachment 1873274
NA ISMAIL MAYUMBA
Dunia kiganjani ni msemo wenye kumaanisha kuwa unaweza kuimiliki dunia na kuiona yote kiganjani mwako kutokana na ukuaji wa utandawazi duniani na kuzidi kupunguza ukubwa wa kuelezea utandawazi kwani zamani walikuwa wanasema dunia imekuwa kama kijiji ila saivi dunia imekuwa kiganjani mwa mtu kwani mtu akiwa ameshika kifaa chochote cha utandawawazi anaweza kufanya jambo lolote na kwa usahihi. Dunia ikiwa kiganjani ina faida na hasara. Kwani ukifungulia dirisha upate upepo jua utaingiza na vidudu ambavyo havionekani kwa macho na vyenye madhara kwako na huo msemo unakuja hadi kwa utandwazi ingawa umeleta faida nyingi pia kuna hasara.
Nafungua dirisha kupata upepo wa kuniburudisha (Faida za utandawazi Tanzania)
Umerahisisha mawasiliano na usafiri.
Vyombo bora za usafiri zimegundulika duniani na kuimarisha njia za usafiri. Mfano wa vyombo vya usafiri ni treni za umeme, ndege za kisasa, magari ambayo yanatumia umeme. Hivyo vyote na vinginevyo vimefanya usafiri uwe mrahisi na ukiongezea kwenye upande wa mawasiliano pia zimegunduliwa simu zenye uwezo mkubwa wa kufanya kazi nyingi na kuhifadhi kazi za kiofisi. Tanzania haija mgongo utandawazi kwani awamu ya tano ya uongozi ikiongozwa na John Magufuli imeweza kuleta miradi usafiri kama kutengeneza miondumbinu ya umeme ambapo treni za umeme zitaitumia na pia ameleta ndege nane na Rais Samia kaongeza tatu ili kuendana na utandawazi. Kwenye mawasiliano serikali imeziunga kampuni za mawasiliano na kuzipa kodi nafuu ili kujiendesha na kuruhusu vifaa bora vya mawasiliano kuja nchini. Tofauti na nchi nyingi, Tanzania haijafungia mtandao wowote wa kijamii hivyo kuwapa fursa watanzania kujielezea zaidi
Ukuaji wa demokrasia
Uhuru wa vyombo vya habari, kuwepo kwa vyama vyingi vya siasa na kubadilishana kwa madaraka hizo zote ni sifa za kuwepo kwa demokrasia nchini. Tanzania imekuwa mfano bora katika hili kwa awamu ya sita kutoa uhuru kwa vyombo vya habari kwani vinaweza kukosoa hadi viongozi wa juu kama wakifanya mambo ambayo siyo sahihi. Wawakilishi waliopo bungeni na wao wamepewa uhuru na Rais Samia kukosoa vikali pale mawaziri wakileta vitu ambavyo havieleweki. Kikubwa zaidi ni kubadilishana kwa madaraka kwa njia ya amani na hili limeonekana pale Rais wa awamu ya tano alipotutoka duniani na madaraka kupewa mama Samia Hassan bila fujo zozote na hapo nchi yetu ilionesha imekomaa kidemokrasia.
Kwenye kupata upepo kuna vidudu visivyoonekana kwa macho vinaingia na vyenye madhara (Hasara za utandwazi)
Mmomonyoko wa maadili na ukoloni mamboleo
Kabla ya utandawazi ilikuwa vigumu kwa mataifa ya magharibi kuleta utamaduni wao nchini ambao asilimia kubwa hauendani na utamaduni wa Tanzania ila kuja kwa utandawazi umewezesha mataifa ya magharibi kupitisha utamaduni wao kwa kupitia mitandao ya kijamii, filamu na nyingine nyingi. Ukuaji wa utandawazi umesababisha kupotea kwa utamaduni halisi wa Tanzani na maadili ya watu kushuka. Ukoloni tuliotawaliwa hapo awali ulikuwa wa kimabavu kwa kutawaliwa na wao ndo wakiwa viongozi na kulazimisha watanzania kufanya mambo ambayo wanataka kwa nguvu. Ukuaji wa utandawazi umeendelea na ukoloni ila sio kwa kutumia mabavu bali kutumia akili, sio kwa kutawala nchini bali kutawala kwa kutumia migongo ya viongozi wazawa, sio kwa kulazimisha kufanya mambo yao bali huyapamba mambo yao na kwa hiari watanzania huyafata.
Hizo ni baadhi ya faida na hasara za utandawazi ila zipo nyingi. Cha muhimu kuzipa kipaumbele faida za utandawazi na kujua jinsi gani tunaziondoa hasara za utandawazi ili tutumie utandwazi kuiendeleza nchi yetu kiuchumi na kijamii

Upvote
2