Baadhi ya game wanazocheza watoto kwenye simu zinawawezesha kuwasiliana na watu wasiowajua. Unajua anaongea na nani?

Baadhi ya game wanazocheza watoto kwenye simu zinawawezesha kuwasiliana na watu wasiowajua. Unajua anaongea na nani?

Cute Wife

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2023
Posts
1,906
Reaction score
5,000
Wakuu salam,

Wakati tunaongea mambo mengine tukumbushane mara moja upande wa malezi ya watoto hasa kipindi hiki ambako digitali inaenda kasi.

Watoto wengi wakati huu wapo exposed kwenye ulimwengu wa digitali kupitia TV, simu, laptops, magemu nk. Leo tuongelee upande huu wa games, ambayo yapo ya aina nyingi, kuna zile unaweza kupakua kupitia simu au laptop, na kuna zile aina ya PS4, 5 na zinazofanana na hizo ambazo unaunganisha na tv na kuburudika.

Wengi wamezoea kuona hayo kwenye game kama PS4, 5, Roblox, nk ndio zenye uwezo wa kusaliana na watu wengine (interactive games), lakini pia kuna games nyingine kama za karata, cross word puzzle, nk, ambazo zinazonekana ni za kawaida tu lakini zina sehemu ya kutuma ujumbe zinazomuwezesha mtu kutuma namba ya simu na kupata taarifa nyingi za anayehusika kucheza game hiyo mahali anapoishi, anaishi na nani, ni familia ya aina gani, anapendwa na wazazi wake au lah, shule anayosoma, kama ana mpenzi au la, kupanga miadi ya kuonana na kumfundisha mambo mengi ya ajabu, na hapa tunaongelea watoto.

Umeshawahi kumuuliza mtoto wako anaependelea game gani kwenye simu ukapitia ukaangalia kama game hiyo ni salama kwake au la? Kuna game nyingi za kuwafaa watoto lakini pia zenye ushenzi hazikosekani.

Kama ulikuwa unachukulia poa, toa muda wako hapa kufatilia nini anapendelea kufanya ili uhakikishe mtoto wako yupo salama na anatumia kifaa cha kidigitali kwa matumizi sahihi na salama kwake.
 
Hapa cha msingi ni kukaa chini na mwanao umuelimishe jinsi ya kutumia mitandao. Kubwa kuliko yote ni kuto entertain mawasiliano na watu asiowajua.
 
Back
Top Bottom