DOKEZO Baadhi ya Halmashauri za mkoa wa Geita zinawaibia watumishi posho zao kwenye uchaguzi, TAMISEMI fuatilieni

DOKEZO Baadhi ya Halmashauri za mkoa wa Geita zinawaibia watumishi posho zao kwenye uchaguzi, TAMISEMI fuatilieni

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Wakati baadhi ya Halmashauri zikitenda haki kwa watumishi na kufuata miongozo ya TAMISEMI katika zoezi, tumebaini kuna baadhi ya Halmashauri kazi ya upigaji na kujitajirisha watu wachache kwa kutumia stahiki za 'wanyonge' inafanyika kama vile ni mashindano. Yaani wasimamizi wa uchaguzi wilaya (DEDs) na maafisa uchaguzi pamoja na majopo yao wanashindana kuwapiga wasaidizi wao wa kata na vijiji katika maeneo yao. Sijui kama wizi huo una baraka kutoka kwenu au ndo mbinu za wasaidizi kumharibia mama.

Mchengerwa chukua hatua.

Watumishi hawalipwi stahiki zao. Hawalipwi fedha za uhamisho, fedha za likizo, fedha za kujikimu, mafao ya uzazi nk kwa amani, hadi vita ya kutosha ipiganwe. Madaraja na miundo inabadilishwa kwa connection nk, vituo vizuri vya kazi vinanunuliwa kimichongo mtu anashtukia anahamishwa tu inaingia njemba nyingine, na fedha ya uhamisho halipwi pia!

Sasa wameona haitoshi, na uchaguzi uhujumiwe. Chaguzi za nyuma wizi ulikuwepo, ila term hii sasa imekuwa too much! Bado ni mwanzo tu lakini speed ya dhuluma ni kubwa sana, hadi kufika tarehe 27/11 watu watakuwa wamekamuliwa sana. Ikiwezekana toeni mwongozo wa malipo uwe wazi kwa wahusika wote nchi nzima, na kama kila halmashauri in discretional power ya kuamua viwango vyake vya posho awamu hii basi iwekwe wazi mapema.

Mchelea mwana kulia hulia mwenyewe. Baadaye msiseme hamkuambiwa.
 
Back
Top Bottom