KERO Baadhi ya Hospitali za Bagamoyo zinalazimisha Wagonjwa kununua dawa na vifaa vya upasuaji hospitalini kisa ushindani wa kibiashara

KERO Baadhi ya Hospitali za Bagamoyo zinalazimisha Wagonjwa kununua dawa na vifaa vya upasuaji hospitalini kisa ushindani wa kibiashara

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Anonymous

Senior Member
Joined
Apr 6, 2006
Posts
118
Reaction score
339
Mimi ni mfanyabiashara wa dawa za binadamu (pharmacy) katika Wilaya ya Bagamoyo. Ningependa kuwasilisha changamoto kubwa inayowakumba wagonjwa wanaotibiwa katika hospitali ya wilaya hiyo.

Changamoto hii inahusiana na utaratibu wa hospitali kushurutisha wagonjwa kununua dawa na vifaa vya upasuaji moja kwa moja hospitalini, hata pale ambapo wagonjwa wameamua kununua nje ya hospitali kutokana na unafuu wa bei.

Tatizo linakuwa kubwa zaidi pale ambapo mgonjwa yupo tayari kwenye chumba cha upasuaji na amekuja na vifaa vilivyonunuliwa nje ya hospitali na hizo dawa zimeandikwa kwenye cheti kabisa.

Wagonjwa wanalazimishwa kurudi kununua vifaa hivyo upya hospitalini kwa gharama mara mbili zaidi, hali inayosababisha mateso ya kifedha na usumbufu mkubwa kwao.

Na inakuwa usumbufu pia kwa wenye pharmacy kwakuwa wateja wanakuja kuomba warudishe dawa ambazo kimsingi zinakidhi vigezo. Ingekuwa dawa ime-expire, kuharibika basi inge-make sense. Vita vya kibiashara ipo ndani yake ila hospitali haipaswi kumtesa mgonjwa. Ushahidi wa watu Upo.

Juhudi za kufikisha malalamiko haya kwa Mganga Mkuu hazijazaa matunda, kwani jibu lake limekuwa kwamba anazingatia mapato ya hospitali. Je, tunapaswa kuipa kipaumbele mapato kuliko utu wa binadamu?

Hii ni hali inayohatarisha maisha ya wagonjwa na kuondoa uaminifu kwa taasisi za afya, ambazo kimsingi zinapaswa kuwa kimbilio la watu wanaohitaji msaada wa matibabu. Tunatoa wito kwa mamlaka husika na wahusika wote kuhakikisha kuwa haki za wagonjwa zinalindwa na kuwa upatikanaji wa huduma za afya unazingatia utu na misingi ya kibinadamu.

Asante kwa kuchukua muda wenu kusikiliza. Tunatumaini hatua stahiki zitachukuliwa ili kuboresha hali hii.
 
"Wagonjwa wanalazimishwa kurudi kununua vifaa hivyo upya hospitalini kwa gharama mara mbili zaidi, hali inayosababisha mateso ya kifedha na usumbufu mkubwa kwao."
 
Back
Top Bottom