KERO Baadhi ya huduma kwa wateja Tanzania ni utapeli kwa jicho la pili

KERO Baadhi ya huduma kwa wateja Tanzania ni utapeli kwa jicho la pili

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Huduma kwa wateja ni kipengele muhimu katika kutoa huduma kwa kuwasaidia wateja kupata taarifa au utatuzi wa changamoto wanazokutana nazo.

Lakini hapa nchini baadhi ya makampuni yanayotoa huduma mbalimbali yanatutesa sana yaani ufikiaji tu wa huduma kwa wateja unatumia gharama kubwa na bado tatizo linaweza lisitatuliwe licha ya kwamba wanajitahidi kuwa wastaarabu.

Mfano, huduma kwa wateja ya DSTV Tanzania, yaani kwanza namba zao sio za bure na bado ukipiga itapokelewa automatically na kukuruhusu kufanya machagulio ya huduma unayoihitaji lakini kwenye suala la kuongea na mhudumu hapo watakuwekea mziki ambao licha ya kua hauna ladha lakini bado utarudiwa hata mara sita au saba ndipo mhudumu ataunganishwa! Sasa hapo tunakua tumepoteza salio ambazo ni hela hizo lakini pia muda unakua umepotea kuachana na kwamba tatizo linaweza kutotatulika na kugharimu zaidi.

Na hii tabia sio kwa DSTV pekee ipo kwenye makampuni mengi sana hata CRDB sema wao kidogo wamejitahidi kongole kwao.

Kweli hatupingi kua watoa huduma ya huduma kwa wateja wanatingwa na kazi au simu zinakua nyingi hilo tunalikubali, Lakini basi tunaomba hizo huduma za simu ziwe za bure kama kampuni au mataasisi mengine ambapo hata kama sina salio la kupiga nitawapata watoa huduma kupitia namba za bure ila hii ya kutumia gharama zetu na bado wanatuwekea muziki mpaka dakika 10 huku wakitusisitiza tusikate inakua ni UTAPELI kwa jicho la pili.

Screenshot_20241029_094652.jpg
 
Ni changamoto kwakweli, ukiwakuta kwenye wiki ya huduma ya wateja wanavyojishembendua utadhani wa maana kweli.
 
Back
Top Bottom